Home LOCAL UFARANSA KUFANYA UWEKEZAJI WA DOLA BILIONI 4.2 NCHINI TANZANIA

UFARANSA KUFANYA UWEKEZAJI WA DOLA BILIONI 4.2 NCHINI TANZANIA

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawamo pichani) wakati wa mkutano maalum na waandishi hao kuzungumzia msafara wa wafanyabiashara kutoka nchini ufaransa waliofika Tanzania kufanya uwekezaji. (kushoto) ni kiongozi wa ujumbe wa wafanyabiashara kutoka Ufaransa.
 

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui (wa nne kulia) akiwa na baadhi ya wafanyabiashara hao walipokuwa kwenye mkutano na waandishi wa habari (hawamo pichani) katika makazi yake Mei 17, 2022 Jijini Dar es Salaam.

Afisa Habari Mwandamizi wa Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania Iku Kassege (kushoto) akiwa na Baadhi ya watumishi wa Ubalozi huo wakifuatilia hotuba ya Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui katika mkutano huo.
Kiongozi wa wafanyabiashara kutoka Ufaransa G’erard Wolf (katikati) akielezea mambo mbalimbali ambayo wafanyabiashara hao watakwenda kuyafanyiakazi katika uwekezaji wao hapa Tanzania. (kushoto), ni Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui, na (kulia) ni Pedro Novo kutoka katika jopo la wafanyabiashara kutoka Ufaransa. PICHA NA: HUGHES DUGILO.
 

Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Samwel Shelukindo akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa waandishi wa habari nyumbani kwa Balozi Hajloui Mei 17,2022 Jijini Dar es Salaam.



Baadhi ya waaandishi kutoka katika vyombo mbalimbali vya habari wakifualia mkutano.
 

Na: Hughes Dugilo – DAR ES SALAAM.

Wafanyabiashara kutoka katika Makampuni na Mashirika ya umma 40 kutoka nchini Ufaransa wamefanya ziara nchini Tanzania  kwaajili ya kuangalia fursa za uwekezaji kwenye maeneo mbalimbali ambapo uwekezaji wao unatarajiwa kuwa wa Dola bilioni 4.2.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Mei 17,2022 Jijini Dar es Salaam Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui akiwa na jopo la wafanyabiashara hao amesema kuwa kampuni hizo 40 pamoja  na mashirika ya umma na binafsi ya nchini Ufaransa (Bpifrance, Business France na MEDEF International), wataalamu katika sekta za  usafiri, nishati, maji safi, kilimo, chakula na afya zimekuwa zikiangalia fursa zilizoko nchini ili kukidhi mfumo wa ikolojia wa Tanzania wa umma/binafsi ili kukidhi mahitajiya soko..

“Ziara ya ujumbe huu imechochewa na nia ya dhati ya kampuni za Ufaransa kwa Tanzania, nchi ambayo  kutokana na ukuaji wake wa nguvu na utulivu wa kisiasa, inatoa matarajio makubwa ya maendeleo kwa wataalamu waUfaransa. Fursa hizi zinatia matumaini zaidi kwani nchi inajitahidi kurejesha hali ya biashara inayowafaa wawekezajiwa kigeni.

“Wakati wa mkutano wake na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Ufaransa mjini Paris Februari 14 wakatiwa ziara yake nchini Ufaransa, Rais Samia Suluhu Hassan alisisitiza kuhusu mageuzi yake ya “biashara bora” na akakaribisha makampuni ya Ufaransa kuja nchini Tanzania,”ameeleza Balozi Nabil Hajlaoui.

 Amefafanua miezi mitatu baada ya mwaliko huo  kampuni za Ufaransa ziliitikia kwa wingi mwito huo na walipata heshima ya kukutana na Rais jijini Dar es Salaam na kufanya mazungumza katika maeneo mbalimbali yanayohusu fursa za uwekezaji.

“Ufaransa ambayo kwa sasa inashikilia wadhifa wa Urais wa Umoja wa Ulaya, pia inakusudia kuisaidiaTanzania kuhamasisha vyombo vya ushirikiano wa Ulaya, kama vile mpango wa Global Gateway (hadi Euro bilioni 300 katika uwekezaji) ili kuipa nchi miundombinu bora naendelevu.

“Tunachoweza kueleza kwa sasa ni kwamba idadi ya kampuni za Ufaransa nchini Tanzania imeongezeka zaidi ya mara tatu kuanzia mwaka 2019 hadi 2022 (makampuni 40 mwaka 2022 ikilinganishwa na 12 mwaka 2019). Kwa mantiki hii, inadhirisha kuwa uwepo wa Wafaransa umepanuka lakini pia umetofautiana kuhusiana na  kuongezeka kwa idadi ya biashara ndogo na za kati…

“Na biashara za ukubwa wa kati zinazoungwa mkono na ofisi yakikanda ya Biashara ya Ufaransa, kuongezeka kwa kiwango cha Bpifrance nchini na kuongezeka kwa mamlaka ya Chama cha Wafanyabiashara wa Kifaransa na Watanzania, ambachosasa kina wanachama 40, yakiwemo makundi kadhaamakubwa ya kimataifa,”amesisitiza Balozi huyo.

Ameongeza kwa hivyo kampuni za Ufaransa zitaendelea kuja Tanzania kwa lengo la kuhakikisha wanashirikiana katika mkakati wa muda mrefu na kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya nchi. “Wamethibitisha kuendelea kudumisha uhusiano huu kupitia miradi nauwekezaji wao nchini licha ya changamoto inayohusishwa najanga la Covid-19.

“Kwa hivyo Ufaransa iko mbioni kuwa mwekezaji mkuu wa Ulaya nchini Tanzania, kwa sababu ina nia yakuongeza ushiriki wake wa moja kwa moja katika miradiya maendeleo ya nchi, hasa usambazaji na uzalishaji wanishati kupitia makampuni ya Ufaransa kama vile Engie, Total Energie na Maurel & Prom, usafiri na vifaa,”amesema.

Ameeleza kama vile ushirikiano na Airbus na mradi wa ukarabati wa Terminal 2 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam na Bouygues Bâtiment International.Kampuni za Ufaransa pia yamejipanga katika maeneo mengine kama vile usafiri wa baharini (mradi wa bandari ya Bagamoyo).

ameongeza kuwa pia sekta ya maji na usafi wa mazingira, mawasiliano ya simu(yaliyozinduliwa hivi karibuni na Eutelsat ya huduma yake yamtandao ya kasi ya satelaiti kupitia kampuni tanzu ya KonnectBroadband Tanzania) na afya (mradi wa hospitali) Dodoma; msaada kwa vituo vya saratani  nchini kote).“Hivyo kupitia makubaliano ya ushirikiano katika kipindi cha miaka mitano ijayo uwekezaji wetu utakufa umefikia kiasi cha  dola bilioni 4.2,”amesema Balozi Hajlaoui.

Ujumbe huo wa wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa umetokana na ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyoifanya nchini Ufaransa mwezi Februari 2022 na ziara ya Waziri wa Ufaransa anayeshughulikia Biashara ya Nje na Vivutio vya Uchumi, Franck Riester jijini Dar-es-Salaam Oktoba 2021.

 Mwisho

Previous articleAZAM FC YAIKABA SIMBA CHAMAZI
Next articleYASEMAVYO MAGAZETI ASUBUHI YA LEO ALHAMISI MEI 19-2022
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here