Shaka asema hatua hiyo inatafsri kazi nzuri inayofanywa na serikali ya awamu ya sita Katia kuwahudumia wananchi.
Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimempongeza Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kutwaa tuzo ya Babacar Ndiaye, kutoka Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB).
Tuzo hiyo inatokana na kutambua kazi kubwa ya ujenzi wa miundombinu, iliyofanywa na Tanzania ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuifungua Afrika kimaendeleo.
Akizungumza kwa nyakati tofauti katika soko la samaki ferry na Stendi ya Mabasi ya Mbezi Luis akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Dar es Salaam, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, amesema tuzo hiyo ni matokeo ya kazi nzuri inayofanywa na serikali chini ya Rais Samia.
“Kutambulika na pongezi anazopokea Rais Samia kimataifa ni matokeo ya kazi nzuri anayoifanya na serikali ya awamu ya sita. Tumepata Rais mwenye nia, dhamira na malengo ya kuleta maendeleo,” amesema.
Amesema tuzo hiyo ya Babacar Ndiaye kwa mwaka 2022, ambayo Rais Samia alikabidhiwa na Makamu wa Rais wa Sekta
Binafsi, Miundombinu na Viwanda wa AfDB, Solomon Quaynor kwa niaba ya Rais wa benki hiyo, Dk. Akinumwi Adesina, ni mfululizo wa matukio ya heshima anayoiptia Tanzania.
Shaka amesema mbali na tuzo hiyo, Rais Samia ametajwa kuwa miongoni mwa viongozi 100 wenye mvuto duniani akiwa katika mstari mmoja na Marais Joe Biden wa Marekani, Xi Jimping wa China na viongozi wengine maarufu.
Amewataka Watanzania kuendelea kumuunga mkono Rais Samia ili aendelee kufanikisha mambo makubwa kwa Taifa katika kuwaletea maendeleo wananchi.
Rais Samia amekabidhiwa tuzo hiyo mjini
Accra, Ghana katika hafla iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali.