Na: Heri Shaaban (Ilala)
WANACHAMA wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala wamemchagua Mwenyekiti wa Jumuiya Wazazi Wilaya ya Ilala Mohamed Msophe, aliyeshinda kwa kishindo
Akitangaza Matokeo hayo Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya ya Ilala , Michael Msuya, alisema katika Uchaguzi huo wapiga kura walikuwa 755 kati ya wapiga kura 755 kura zilizopigwa 751 kura nne zimearibika Mohamed Msophe ameibuka mshindi kwa kura 612 na Mpinzani wake Hamis Hamis amepata kura 135 .
Akitangaza matokeo hayo Msuya alisema anamtangaza Mohamed Msophe kwa ushindi nafasi ya Mwenyekiti Wilaya ya Ilala Jumuiya ya Wazazi .
Mohamed Msophe ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi kwa kipindi cha awamu ya pili awali aliongoza nafasi hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu baada nafasi hiyo kuachwa wazi na aliyekuwa Mwenyekiti Lucas Lutainurwa, ambaye kwa sasa ni Diwani wa Gongolamboto.
Msimamizi Msuya alisema katika uchaguzi wa Jumuiya ya Wazazi nafasi zingine ambazo zimegombaniwa ni nafasi za uwakilishi ambapo Mkutano Mkuu Wazazi Taifa FRANK MANG’ATI alibuka kidedea kwa ushindi wa kura 483 na mshindi wa Pili Zayana Rashid kura 202.
Aidha Msuya alisema washindi wengine nafasi tatu Baraza Wazazi wilaya Abdallah Othiman,Emanuel Kimalio na Saphina Hussein,Halmashauri Kuu Wazazi George Mtambalike ambaye amepata kura 739 na Leah Samike kura 190 wakati Nafasi ya Wazazi Mkoa Everlin Mwakatuma amepata kura 267 na Tambwe Rashid Kura 285.
Aidha pia katika Uchaguzi huo nafasi za uwakirishi Wazazi kwenda Umoja wa Wanawake Fatuma Mitego alibuka mshindi kwa 340 na mshindi wa Pili Winfrida Ndibalema aliyepata kura 214 na nafasi ya Uwakirishi Uwakirishi Wazazi kwenda Umoja wa Vijana imechukuliwa na Godfrey Mlay aliyepata kura 331 na Raifa Mohamed amepata kura 207.
Mwenyekiti Mteule wa Jumuiya ya wazazi Wilaya ya Ilala Mohamed Msophe .aliwashukuru Wanachama wake wote wapiga kura kwa kumpa ushindi mnono wa kishindo ngazi ya Wilaya ya Ilala .
Mwenyekiti Mohamed Msophe alisema yeye kwa sasa ndio kiongozi wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala ameomba apewe ushirikiano Ofisi yake ipo wazi wakati wote kwa ajili ya kujenga chama na Jumuiya ya Wazazi .
Msophe alisema yupo tayari kupokea ushirikiano wakati wowote Ili kujenga chama pamoja na Jumuiya ya Wazazi iweze kusonga mbele kwani Jumuiya ya Wazazi ndio Jumuiya kubwa Tanzania .
Awali hotuba yake Mohamedi Msophe, alisema alipokuwa Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo kwa muda alipokaa madarakani uongozi wake ameweza kufufua chama na Jumuiya pamoja na Semina elekezi kila Kata kwa ajili ya kuwajenga viongozi wa matawi na Kata .
Aidha alisema pia vipaumbele vyake vingine alivyovifanya kupanda miti Kila Kata na utunzaji MAZINGIRA na kupewa tuzo na Serikali ya Mazingira , kwa muda wa mwaka mmoja na nusu kujenga Ofisi za Kata za Wazazi Semina na mafunzo ya Siasa na uchumi kwa Matawi na Kata zote za Wazazi Wilaya ya Ilala hivyo akichaguliwa atafanya makubwa zaidi katika kuendeleza Jumuiya hiyo .
Mwisho