Na: WAF – Bungeni, Dodoma.
Serikali imepanga kununua majokofu mapya 103 kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za afya ambavyo vina uhaba wa majofoku.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel akijibu swali liliolizwa na Mhe. Zacharia Issay Mbunge wa Mbulu Mjini kuhusu ni lini Serikali itahakikisha kuwa vyumba vya kuhifadhi maiti nchini vinakuwa na majokofu.
Dkt. Mollel amesema kuwa Hospitali zote 28 za rufaa za Mikoa zina majokofu ya kuhifadhia maiti, pia hospitali 16 za Mikoa zimepewa majokofu mapya kati ya hospitali 28 za Rufaa za Mikoa.
“Serikali inatambua kuwa tatizo kubwa la upungufu lipo kwenye hospitali za Wilaya na vituo vya Afya vipya. Hata hivyo, katika mwaka wa fedha 2022/2023 Serikali imepanga kununua Majokofu 103 kwa ajili yakusambazwa katika vituo vya kutolea huduma za Afya” Amesema Dkt. Mollel.