Home LOCAL SERIKALI KUNUNUA MAJOKOFU 103 YA KUHIFADHIA MAITI.

SERIKALI KUNUNUA MAJOKOFU 103 YA KUHIFADHIA MAITI.

Na: WAF – Bungeni, Dodoma.

Serikali imepanga kununua majokofu mapya 103 kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za afya ambavyo vina uhaba wa majofoku.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel akijibu swali liliolizwa na Mhe. Zacharia Issay Mbunge wa Mbulu Mjini kuhusu ni lini Serikali itahakikisha kuwa vyumba vya kuhifadhi maiti nchini vinakuwa na majokofu.

Dkt. Mollel amesema kuwa Hospitali zote 28 za rufaa za Mikoa zina majokofu ya kuhifadhia maiti, pia hospitali 16 za Mikoa zimepewa majokofu mapya kati ya hospitali 28 za Rufaa za Mikoa.

“Serikali inatambua kuwa tatizo kubwa la upungufu lipo kwenye hospitali za Wilaya na vituo vya Afya vipya. Hata hivyo, katika mwaka wa fedha 2022/2023 Serikali imepanga kununua Majokofu 103 kwa ajili yakusambazwa katika vituo vya kutolea huduma za Afya” Amesema Dkt. Mollel.

Previous articleMILIONI 61.4 ZATUMIKA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA KITUO CHA AFYA NDAGO
Next articleJUMLA YA WATOTO 12,131,049 WAMEPATIWA CHANJO DHIDI YA UGONJWA WA POLIO MEI, 2022
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here