Na:Costantine James, Geita.
Mkoa wa Geita unatarajia kupokea wawekezaji kutoa jiji la Dubai lilipo Falme za kiarabu, pamoja na nchini misri kwa ajiri ya kuja kuwekeza mkoani Geita katika sekita mbalimbali.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa mkoa wa Geita Mhe, Rosemary Senyamule wakati wa kikao kazi na wakuu wa taasisi mbalimbali mkoani Geita amesema wawekezaji hao wanakuja kufanya tathimini ili kuja kuwekeza katika maeneo mbalimbali ndani ya mkoa wa Geita.
Senyamule amesema mkoa wa Geita unavivutio mbalimbali vya uwekezaji ambapo amesema mkoa wa Geita umependekeza kuwapeleka wawekezaji katika halmashauri tatu ambazo ni Geita mji, Chato pamoja na Geita wila.
Mhe, Senyamule amewataka wakurugenzi wa halmashauri hizo kufanya maandalazi ya kutosha ili pindi wawekezaji watakapofika mkoani Geita wapate nafasi yakuwekeza katika halmashauri zao.
Nae Kaimu Katibu Tawala Msaidizi kitengo cha Uchumi na Uzalishaji Charles Chacha amesema wawekezaji hao wanalenga kuja kuwekeza katika mkoa wa Geita katika upande wa Masoko ya Dhahabu, maeneo ya ununuzi wa Dhahabu.
Chacha amesema Mkoa wa Geita ni kinara katika sekta ya madini hivyo wawekezaji wameonesha nia yakuja kuwekeza upande wa uchakataji na usindikaji wa madini pamoja na uchimbaji wa madini.
Amesema wawekezaji hao pia wanalenga kuja kuwekeza katika upande wa afya kwa kuanzisha viwanda vya utengenezaji wa madawa pamoja na vifaa tiba huku katika upande wa kilimo wawekezaji hao wamelenga katika usindikaji na uongezaji wa thamani upande wa mazao yanayilimwa mkoani Geita.