Na: Costantine James, Geita.
Wananchi wa kijiji cha busanda kata ya Busanda katika jimbo la Busanda wilayani Geita wamemuomba mbunge wa jimbo la Busanda Tumaini Magesa kuwasaidia kukamilisha ujenzi wa kituo cha afya cha Busanda ili waondokane na adha yakufata huduma za kiafya umbali mrefu.
Mwenyekiti wa kijiji cha busanda ambae ni kiongozi wa eneo hilo ambapo kituo cha afya kinajengwa Bw.Elias Majula amesema ujenzi wa kituo hicho cha afya ulianza mwaka 2017 kwa nguvu za wananchi.
Amesema mpaka sasa ujenzi unaendeelea kwa kushirikiana na wadau mbalimbali pamoja na ofisi ya mbunge wa jimbo la Busanda ambayo imetoa kiasi cha shilingi milioni 2 zilizotumika katika ununuzi wa tofali.
Bw. Majula amemuoamba Mhe, Mbunge wa jimbo la Busanda Tumaini Magesa kuendelea kuunga Mkono ujenzi huo mpaka pale utakapo kamika ili wananchi waanze kupata huduma kwa urahisi zaidi.
Baadhi ya wakinamama wa kata hiyo wameeleza adha ambayo wanaipata kwa sasa na namna ambavyo wanahitaji msaada wa mbunge wao Katika ukalimishaji wa ujenzi wa kituo hicho.
Kwa Upande wake Mbunge wa jimbo la Busanda Tumaini magesa amewatoa hofu wananchi wa kijiji cha Busanda kuwa ofisi yake itaendelea kusaidia ujenzi wa kituo hicho mpaka pale kitakapi kamilika ili kianze kutoa huduma kwa wananchi.