Home LOCAL MBUNGE ATIA NGUVU UJENZI WA KITUO CHA AFYA GEITA.

MBUNGE ATIA NGUVU UJENZI WA KITUO CHA AFYA GEITA.

Na: Costantine James, Geita.

Wananchi wa kijiji cha busanda  kata ya Busanda katika jimbo la Busanda wilayani Geita  wamemuomba mbunge wa jimbo la Busanda Tumaini Magesa kuwasaidia kukamilisha ujenzi wa kituo cha afya cha  Busanda ili waondokane na adha yakufata huduma za kiafya umbali mrefu.

Mwenyekiti wa kijiji cha busanda ambae ni kiongozi wa eneo hilo ambapo kituo  cha afya kinajengwa Bw.Elias Majula amesema ujenzi wa kituo hicho cha afya ulianza mwaka 2017  kwa nguvu za wananchi.

Amesema mpaka sasa ujenzi unaendeelea kwa kushirikiana na wadau mbalimbali  pamoja na ofisi ya mbunge  wa jimbo la Busanda ambayo imetoa kiasi cha shilingi milioni 2 zilizotumika katika ununuzi wa tofali.

Bw. Majula amemuoamba Mhe, Mbunge wa jimbo la Busanda Tumaini Magesa kuendelea kuunga Mkono  ujenzi huo mpaka pale utakapo kamika ili wananchi waanze kupata huduma kwa urahisi zaidi.

Baadhi ya  wakinamama wa kata hiyo wameeleza adha ambayo wanaipata kwa sasa na namna ambavyo wanahitaji msaada wa mbunge wao Katika ukalimishaji wa ujenzi wa kituo hicho.

 Kwa Upande wake Mbunge wa jimbo la Busanda  Tumaini magesa amewatoa hofu wananchi  wa kijiji cha Busanda kuwa ofisi yake itaendelea kusaidia ujenzi wa kituo hicho mpaka pale kitakapi kamilika ili kianze kutoa huduma kwa wananchi.

Previous articleDC ILALA KUZINDUA KUPIMA AFYA BURE ILALA
Next articleTEMBO WARRIORS WAASWA KUWEKA UZALENDO NA UTAIFA MBELE
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here