Home SPORTS TEMBO WARRIORS WAASWA KUWEKA UZALENDO NA UTAIFA MBELE

TEMBO WARRIORS WAASWA KUWEKA UZALENDO NA UTAIFA MBELE

Na: mwandishi wetu.

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo  Mhe. Mohamed Mchengerwa amewataka wachezaji wa timu ya taifa ya watu wenye ulemavu (Tembo Warriors) kuonyesha uzalendo na utaifa kwenye mioyo yao ili kufanikiwa katika mashindano wanayojiandaa nayo ya dunia yanayotarajiwa kufanyika mwaka huu 2022 nchini Uturuki.

Ameyasema  katika hafla ya kuwakabidhi bendera wachezaji wa Tembo Warriors ambao wanaelekea nchini Polland  leo kwa ajili za mechi za majaribio za kimataifa nchini humo kujiweka vizuri kwa ajili ya kombe hilo la dunia kwa kundi hilo nchini Uturuki.

“Serikali na watanzania tunahitaji kuona vitendo na ushindi, serikali itakuwa nanyi baga kwa bega,”alisema Mhe. Mchengerwa.

Aliendelea kwa kuwataka kuendelea kutumia vipaji walivyonavyo kuyabadili maisha yao pamoja na kuiletea sifa nchi kwa kuleta ushindi katika mshindano hayo ya Polland na Uturuki. Lakini pia, ameeleza kuwa Serikali imejipanga kuipa nguvu zaidi michezo inayofanya vizuri.

“Nendeni Mkalete ushindi nyumbani,  Iwapo kila mtanzania akiamua kubadilisha maisha yake inawezekana”alisema Mhe. Waziri.

Waziri Mchengerwa amewataka wachezaji hao kuonesha nidhamu, kujituma uwanjani na kuhakikisha wanafuata maelekezo ya walimu wao ili kufanikiwa katika nafasi waliyopata.

“Hii ni golden chance ambayo wengine wameshindwa kuipata, naomba mkaitumie vizuri, nina imani kuwa mkijipanga lazima mlete kombe nchini”alisema.

Aliongeza kwa kuwaeleza kuwa, watakaporejea wataenda bungeni kama ilivyokuwa kwa timu ya wanawake u17, Serengeti Girls.

Awali Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abassi kabla ya kumkaribisha Waziri Mchengerwa alimweleza kuwa wachezaji hao ndio wamefungua mlango wa kuelekea kombe la dunia kabla ya kufuatiwa na timu ya wanawake ya Serengeti Girls U 17.

Kwa upande wake Rais wa Chama cha Mchezo huo nchini (TAFF) Peter Sarungi ameishukuru Serikali kwa kuiweka timu hiyo kambi muda mrefu tangu Februari mwaka huu, na kuahidi kuwa watarudi na ushindi kuanzia Polland hadi Uturuki.

Naye Kocha wa timu hiyo Evo Mapunda ameihakikishia Serikali kuwa timu itafanya vizuri na kueleza kuwa hata mazoezi yao yamelenga kufanikiwa.

Previous articleMBUNGE ATIA NGUVU UJENZI WA KITUO CHA AFYA GEITA.
Next articleSUSAN BUFFET FOUNDATION KUIPATIA TANZANIA DOLA MILIONI 15 KWA AJILI YA HUDUMA ZA AFYA YA UZAZI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here