Home BUSINESS BENKI YA NBC YATOA SH.50 MILIONI KUSAIDIA UJENZI WA KIWANJA CHA KISASA...

BENKI YA NBC YATOA SH.50 MILIONI KUSAIDIA UJENZI WA KIWANJA CHA KISASA CHA SOKA SINGIDA

Mkurugenzi wa Masoko wa Benki ya Taifa ya Biashara Tanzania (NBC), David Raymond (wa tatu kutoka kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk.Binilith Mahenge, mfano wa hundi yenye thamani ya Sh.50 Milioni iliyotolewa na benki hiyo kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Uwanja wa Soka utakaojengwa eneo la Mtipa nje kidogo ya Manispaa ya Singida katika hafla iliyofanyika leo mjini Singida. Wengine kutoka kushoto ni Mtahiki Meya wa Manispaa ya Singida, Yagi Kiaratu, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Singida, Alhajj Juma Killimbah Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskas Mulagiri na Meneja wa Benki ya NBC Mkoa wa Singida, Asia Chembaga.
 
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk.Binilith Mahenge, akizungumza wakati wa kupokea msaada huo.
 
Mkurugenzi wa Masoko wa Benki ya Taifa ya Biashara Tanzania (NBC), David Raymond akizungumza kabla ya kukabidhi fedha hizo.
 
 Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskas Mulagiri akizungumza kwenye hafla hiyo.
 

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Alhajj Juma Killimbah akizungumza kwenye hafla hiyo.

Meneja wa Benki ya NBC Mkoa wa Singida, Asia Chembaga akizungumza .

Baadhi ya Wafanyakazi wa Benki ya NBC Mkoa wa Singidawakiwa kwenye hafla hiyo
Wadau wa michezo mkoani hapa wakiwa kwenye hafla ya kukabidhiwa fedha hizo.
 
Hafla hiyo ikiendelea.
 
Afisa Utamaduni Mkoa wa Singida Henry Kapela akiongoza hafla hiyo.
 
Viongozi mbalimbali wakiwa meza kuu wakati wa hafla hiyo. Kushoto ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida, Yagi Kiaratu.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk.Binilith Mahenge (wa pili kutoka kushoto) na viongozi pamoja na wadau wa michezo na maafisa Ardhi wakiangalia ramani ya uwanja huo utakao jengwa eneo la Mtipa. 

Na: Dotto Mwaibale, Singida

BENKI ya Taifa ya Biashara Tanzania (NBC) imetoa Sh. 50 Milioni kwa ajili ya kuisaidia ujenzi wa kiwanja cha kisasa kitakacho jengwa eneo la Mtipa nje kidogo ya Manispaa ya Singida.

Kiwanja hicho kitakuwa kikimilikiwa na Timu ya Singida Big Star ambayo imeingia msimu huu kushiriki mashindano ya Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kupanda daraja.

Akizungumza wakati wa hafla ya kupokea fedha hizo Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk.Binilith Mahenge ameishukuru benki hiyo kwa kusikia kilio cha muda mrefu cha wadau wa michezo mkoani hapa na kukubali kuchangia kiasi hicho cha fedha.

“Maombi ya wadau wa mkoa, chama na wawakilishi wetu Bbenki ya NBC wameyasikia na kuamua kutupatia kiasi hiki cha fedha hongereni sana NBC tutahakikisha fedha hizi zinakwenda kufanya kazi iliyokusudiwa na si vinginevyo” alisema Mahenge.

Mahenge alisema anatamani sana kuona sasa kuna kuwa na mechi za mfululizo zikifanyika katika uwanja wa zamani na huo mpya ukikamilika ili wananchi wa Mkoa wa Singida wafaidike kwa kupata burudani ya mechi mbalimbali.

Alisema kujengwa kwa viwanja vingi vya michezo kutafungua fursa kwa wafanyabiashara wenye mahoteli na makundi mengine ya kupata fedha na hata kuhufanya mji wa Singida kupanuka.

Dk. Mahenge alisema kukamilika kwa viwanja hivyo ambavyo vitajengwa eneo hilo la Mtipa na  pembeni mwa barabara ya kutoka Singida kwenda Arusha vitapendezesha mji wa Singida na kuwa kimbilio la wageni kwenda kupumzika kutokana hewa nzuri inayopatika mkoani humo.

Aidha Dk.Mahenge aliendelea kuipongeza benki hiyo kwa kujitoa kuisadia Serikali na kueleza kuwa hata alipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma alishuhudia benki hiyo ikitoa msaada mkubwa na hata magari na alitumia nafasi hiyo kuwaeleza kuwa Serikali mkoani hapa itaendelea kushirikiana nayo ambapo alitoa wito kwa timu ya Singida Big Star itakayosimamia ujenzi wa kiwanja hicho kuhakikisha kinajengwa kwa viwango kutokana na eneo kilipo kiwanja hicho kuhitaji utaalamu na kuwa wahandisi wa mkoa na Mkuu wa Wilaya ya Singida ambaye ni Mhandisi wataipitia michoro ili ujenzi huo uwe sawasawa.

Akikabidhi msaada huo kwa niaba ya mkurugenzi mkuu wa benki hiyo, Daudi Raymond ambaye ni Mkurugenzi wa Masoko wa benki hiyo alisema wamekuwa wakitoa huduma za kibenki mkoani hapa  kwa miongo mingi na kuwa wanajivunia kuwa wa kwanza.

Alisema benki hiyo ni mdau mkubwa wa maendeleo hapa nchini  kama kauli mbiu yao inavyosema daima karibu nawe tunathaamini umuhimu wa kuwa karibu na wateja wetu, wadau na jamii kwa ujumla.

Alisema sera yao ya kurudisha faida wanayoipata kwa jamii imejikita katika sehemu kuu tatu, elimu, afya ya mama na mtoto pamoja na maendeleo ya jamii ikiwemo michezo mbalimbali.

Raymond alisema katika kipindi cha mwaka uliopita benki hiyo iliweza kusaidia zaidi ya Sh.Bilioni 1 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya kijamii na kiasi hicho ni nje ya Sh.9 Bilioni waliyotoa kwa ajili ya kudhamini Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa kipindi cha misimu mitatu.

Alisema wanajivunia kushiriki maendeleo ya soka hapa nchini  na kuwa wataendelea kutoa michango kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya michezo kama soka, riadha, gofu na mingine mingi na kuwa benki hiyo inaamini kuwa michezo ni afya na ajira hivyo wanafuraha kubwa kukabidhi kiasi hicho cha fedha ambazo zimelenga kuboresha uwanja wa michezo na matumaini yao kuwa mchango huo utasaidia kuinua  na kuibua vipaji vya michezo mkoani Singida.

Raymond alitumia nafasi hiyo kuwakaribisha wakazi wa Singida kwenye tukio mashuhuri la Dodoma NBC Marathoni ambalo Kitaifa litafanyika Julai 31, 2022 kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma lenye lengo ya kukusanya fedha kwa ajili ya kongamano la saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake ambapo wanashirikiana na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Alhajj Juma Killimbah alisema ujenzi wa viwanja hivyo ni utekelezaji wa Ilani ya chama hicho katika kudumisha michezo hapa nchini kwani chama hicho kilianza zamani kuvijenga na ndio maana vipo katika mikoa yote.

 

Previous articleMAGHETO CHANZO CHA UKATILI WA KIJINSIA …WANAFUNZI LUNGUYA SEKONDARI WAVUNGA KURIPOTI HOFU YA VITISHO, KUROGWA
Next articleRC SINGIDA AZINDUA GHALA LA KISASA NA KUWATAKA WAKULIMA KUFANYA KILIMO BIASHARA, DC MURO AWA MBOGO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here