Home LOCAL WATOTO 263,990 WANATARAJIA KUPATA CHANJO YA POLIO MKOANI PWANI-DKT.GUNINI

WATOTO 263,990 WANATARAJIA KUPATA CHANJO YA POLIO MKOANI PWANI-DKT.GUNINI

Na: Mwamvua Mwinyi,Pwani
MKOA wa Pwani unatarajia kuchanja watoto wote wenye umri chini ya miaka mitano wapatao zaidi ya 263,990 ili kuwakinga na ugonjwa wa polio kwa utoaji wa matone.
Hayo yalisemwa Mjini Kibaha na Mganga Mkuu wa Mkoa huo,Dkt. Gunini Kamba wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kampeni ya utoaji wa matone ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa Polio.
Kamba alisema kuwa kampeni hiyo ya utoaji matone itakuwa ya siku nne ambapo lengo ni kuhakikisha watoto wote wanaostahili kupata chanjo wanapatiwa chanjo hiyo kwa wale wote wenye umri chini ya miaka mitano .
“Mkoa ulifanya vizuri katika awamu ya pili kwa Kuvuka lengo la Uchanjaji kwa kufikia jumla ya watoto walio na umri chini ya miaka mitano 263,851 ambayo ni  asilimia 131.2 ya walengwa wote na hivyo wanatarajia kufanya vizuri zaidi katika awamu hii ya tatu.”
“Naomba nitoe rai kwa viongozi na watendaji wote wa Serikali, vyama vya Siasa, Dini, Taasisi na Wadau wote katika kuhakikisha tunashirikiana kikamilifu na kuhakikisha jamii yetu hususani wazazi na walezi wa watoto wanapata taarifa sahihi juu ya zoezi hili na umuhimu wake kwa afya za watoto wetu,”alisema Kamba. 
Nae mratibu wa chanjo Mkoani hapo , Abbas Hincha alisema katika kuhakikisha kila mtoto anafikiwa timu za uchanjaji zitapita nyumba kwa nyumba na sehemu yoyote ile walipo watoto sokoni, shule za chekechea, nyumba za ibada na Kauli mbiu inasema kila tone la chanjo ya polio litaiweka Tanzania salama dhidi ya ugonjwa wa kupooza.
Alieleza, chanjo hiyo siyo mara ya kwanza kutolewa hapa nchini hivyo wazazi wahakikishe watoto waliolengwa wanafikiwa na chanjo hiyo .
Previous articleKINANA AKAGUA MRADI UJENZI WA GATI LA BANDARI YA UJIJI MKOANI KIGOMA
Next articleRAIS SAMIA AHANI MSIBA WA MTOTO WA MZEE MWINYI CHUKWANI ZANZIBAR
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here