Wafanyakazi wa Kampuni ya Usafi ya Kajenjele wakiwa katika kampeni endelevu ya Usafi ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Eneo la Gerezani Leo Agosti 27/2022 (PICHA NA SHAABAN)
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ludigija na Meya wa Halmashauri ya Jiji Omary Kumbilamoto wakiwa katika usafi Kata Gerezani Leo Agosti 27/2022 (PICHA NA HERI SHAABAN)
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ludigija na Meya wa Halmashauri ya Jiji Omary Kumbilamoto wakiwa katika usafi Kata ya Gerezani Leo Agosti 27/2022 (Kulia)Mkandarasi wa Kampuni ya Usafi Kajenjele na Mwenezi wa CCM Gerezani Athumani Chila (Picha na Heri Shaaban)
Diwani wa Kata ya Gerezani Fatuma Abubakari (Katikati)akiwa na Afisa Mazingira Rajabu Ngoda (kushoto)katika kampeni endelevu ya usafi Kata ya Gerezani Leo Agosti 27/2022(PICHA NA HERI SHAABAN)
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ludigija na Meya wa Halmashauri ya Jiji Omary Kumbilamoto wakiwa katika usafi Kata Gerezani Leo Agosti 27/2022 (PICHA NA HERI SHAABAN)
Na: Heri Shaaban (Ilala)
MKUU wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ndatwa Ludigija amesema Wilaya ya Ilala inatarajia kuanza Oparesheni ya kuwakamata wazalishaji wa mifuko ya nailoni ndani ya Wilaya ya Ilala .
Mkuu wa Wilaya Ludigija alisema hayo Dar es Salaam Leo katika Oparesheni endelevu ya Usafi Kata ya Gerezani Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ambapo Wananchi wameshiriki usafi ,Wafanyabiashara na Viongozi wa chama Kata ya Gerezani akiwemo Diwani wa Gerezani Fatuma Abubakari ,Diwani wa Viti Maalum Wilaya ya Ilala AISHA JOHARI na Meya wa Halmashauri ya Jiji Omary Kumbilamoto.
“Jumatatu tunaanza Oparesheni Maalum ilala kuwakamata wazalishaji mifuko laini ya nailoni ambayo inachafua Mazingira Wilayani kwetu tutawakamata na kuwachukulia hatua “ alisema Ludigija .
Mkuu wa Wilaya Ludigija alisema Wilaya ya Ilala wameshakaa vikao na wadau wakiwemo TBS,TFDA Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya kwa ajili ya kutekeleza maagizo ya Serikali kwa ajili ya kuweka Halmashauri ya Jiji katika hali ya usafi
Aidha alisema wameshatoa elimu katika masoko yote wasiendelee kutumia mifuko laini ikiwemo katika vifungashio
Alisema kampeni ya usafi ni endevu mwananchi unatakiwa kuchukia uchafu halmashauri ya Jiji ni Jiji la mkakati kwa ajili ya kukuza uchumi wa nchi yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Pia alisema Ilala tayari kuanzia Leo stika za matangazo zinabandikwa kwa ajili ya kuzuia mifuko ya lain ya nailoni.
Katika hatua nyingine Ludigija amempongeza Kampuni ya usafi ya Kajenjele kwa kuboresha Jiji kwa usafi pamoja na kampuni zingine.
Meya wa halmashauri ya Jiji Omary Kumbilamoto alisema Maelekezo ya Mkuu wa mkoa katika halmashauri ya Jiji watatekeleza pamoja na madiwani wa Halmashauri hiyo.
Diwani wa Gerezani Fatuma Abubakari alimpongeza Mkuu wa Wilaya pamoja na Mkuu wa mkoa Kata ya Gerezani Leo kufanya usafi ngazi ya Wilaya .
Mwisho