Home LOCAL BILIONI 6 ZIMETENGWA KUBORESHA MIUNDOMBUNU YA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA HOSPITALI YA...

BILIONI 6 ZIMETENGWA KUBORESHA MIUNDOMBUNU YA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA SHINYANGA


Na: WAF Bungeni, Dodoma.

Katika mwaka ujao wa fedha 2022/23 Serikali imetenga shilingi Bilioni 6 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya kutolea huduma za afya ikiwemo na huduma za Watoto njiti katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel leo Bungeni Jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na Mbunge Viti Maalum Mhe. Santiel Kirumba aliyeuliza ni lini Serikali itaboresha Kitengo cha Watoto Njiti katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Akijibu swali hilo kuhusu Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Dkt. Mollel amesema Hospitali hiyo kwa sasa ina sehemu maalum yenye uwezo wa kulaza Watoto njiti 18 kwa wakati mmoja.

“Serikali inaendelea na ujenzi wenye thamani ya Bilioni 1.2 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga utakaowezesha hospitali hiyo kuwa na vitanda 42 vya kulaza Watoto njiti na kwenye bajeti ya mwaka 2022/2023 zimetengwa shilingi bilioni 6 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga” amesema Dkt. Mollel.

Previous articleMEYA KUMBILAMOTO ATAKA FAHARI WAUNGWE MKONO KUKOMESHA UKATILI KWA WATOTO
Next articleTUTAENDELEA KUHAKIKISHA UPATIKANAJI WA DAWA NA VIFAA TIBA KWA WANANCHI – WAZIRI. UMMY
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here