Home LOCAL INASIKITISHA WATOTO 2 WAMEUWAWA KIKATILI KWA KUBAKWA KISHA KUJICHJWA WILAYANI NYANG’HWALE...

INASIKITISHA WATOTO 2 WAMEUWAWA KIKATILI KWA KUBAKWA KISHA KUJICHJWA WILAYANI NYANG’HWALE GEITA

Na.Costantine James, Geita.

Watoto wa wili  Nkeya Thomas( 2), Dorcas Thomas( 7) wameuwawa Kikatili wilayani Nyang’hwale Mkoani Geita kwa kubakwa kisha kujichwa hali iliopelekea kupoteza uhai wao.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Geita  Kamishina Msaidizi Henry Mwaibambe amedhibotisha kutokea kwa matukio hayo yaliyotokea wilaya ya Nyaghwale Mkoani Geita ndani ya wiki moja.

Mwaibambe amesema Jeshi hilo linawashikilia watu wane, wakazi wa kata ya Ibambila wilayani Nyanghwale, watatu wa familia moja na mmoja mganga wa kienyeji kwa tuhuma za kumbaka na kumuua  Dorcas Mathias  mtoto wa miaka 7, huku wakihusishwa na Imani za kishirikina.

Kamanda Mwaibambe amesema waliwakamata vijana wawili wa familia moja na mganga wa kienyeji lakini badae waliamua kumkamata mama wa watuhumiwa wawili baaada ya kuitishia familia iliyofiwa kuwa atakufa tena mtoto mwingine katika familia hiyo.

Mwaibambe amesema tukio hilo limetokea majira ya mchana huku akiwataka wakazi wa Ibambila kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo ili kuhakikisha wahusika wahusika tukio hilo wanakamatwa na kufikishwa mahakani.

Aidha Mwaibambe amesema Jeshi hilo Jeshi la Polisi mkoani Geita limefanikiwa  pia  kuwakamata watu watano kwa tuhuma za mauaji ya Nkeya Thomas (2) ametumia nafasi hiyo kuwataka wananchi kucha mara moja kujihusisha na mauji kwani nikinyume na sheria na wale wote watakoa bainika kufanya vitendo hivyo wataadhibiwa kwa mji wa sheria za nchi.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Geita Rosemary Senyamule amelani mauji hayo amesema hakuna mtu yoyote mwenye haki ya kutoa uhai wa mtu mwenzie serikali haitawavumilia.

Senyamule amesema vipo viashiria vya mauaji ya watoto hao wawili kuwa ni vitendo vya kishirikina
Mkuu wa mkoa wa Geita ameiagiza idara inayohusika kusajili waganga wa jadi wilayani humo kuwatambua waganga halali ili kuwaondoa wanapiga ramli chonganishi ili kuondoa vitendo vya mauaji yanayotokana na Imani za kishirikina.

Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Ibambila wameiomba serikali kufanya uchunguzi uchunguzi wa haraka juu ya mauaji hayo ili wahusika wa vitendo hivyo wachukuliwe hatu kwa mjibu wa sheria hali itakayosaidia kumaliza mauaji ndani ya wilaya ya Nyang’hwale.

Previous articleSTAR TIMES, THE LOOK WAPEWA PONGEZI BASATA
Next articleWAMASAI WAFANYA MAANDAMANO YA AMANI KATIKA UBALOZI WA KENYA JIJINI DAR
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here