Home LOCAL WAMASAI WAFANYA MAANDAMANO YA AMANI KATIKA UBALOZI WA KENYA JIJINI DAR

WAMASAI WAFANYA MAANDAMANO YA AMANI KATIKA UBALOZI WA KENYA JIJINI DAR



 Tazama Video 

https://youtu.be/QsoxZ91GvlU 

wamaasai kutoka katika maeneo mbalimbali ya Tanzania wamefanya maandamano ya amani hadi Ubalozi wa kenya tanzania, uliopo oysterbay Jijini Dar es salaam leo juni 17, 2022 kuiomba Serikali ya nchi hiyo iingilie kati upotoshaji unaofanywa na asasi za kiraia na wana harakati katika zoezi la kuhama kwa hiari linaloendelea katika wilaya ya ngorongoro pamoja na tarafa ya loliondo.

wamasai hao wameeleza kuwa upotoshaji huo umelenga kuichonganisha jamii ya wamasai na Serikali ya yao ya Tanzania, pamoja na kuzorotesha jitihada mbalimbali za makubaliano zilizofikiwa na pande zote mbili.

hayo yameelezwa kupitia barua ya pamoja iliyosainiwa na katibu wa umoja huo Bw. loishiye lashilunye iliyosomwa na kiongozi wa msafara aliyejitambulisha kwa jina moja la emanuel.

hatua hii inakuja baada ya zoezi la kuweka alama za mipaka katika eneo la loliondo pamoja na uhamaji wa wananchi wa ngorongoro ambapo licha ya serikali kutanabaisha uwepo wa makazi mapya katika eneo la handeni, kumetokea upotoshaji na uchochezi unaolenga kukwamisha zoezi hilo.


Previous articleINASIKITISHA WATOTO 2 WAMEUWAWA KIKATILI KWA KUBAKWA KISHA KUJICHJWA WILAYANI NYANG’HWALE GEITA
Next articleTIGO WATOA MILIONI 10 KWA MSHINDI WA ” TIGO CHEMSHA BONGO “.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here