Home BUSINESS BAADHI YA DONDOO ZA VIONGOZI WALIOZUNGUMZA KATIKA HAFLA YA UZINDUZI WA MNADA...

BAADHI YA DONDOO ZA VIONGOZI WALIOZUNGUMZA KATIKA HAFLA YA UZINDUZI WA MNADA WA KWANZA WA MADINI YA VITO, MIRERANI – DESEMBA 14, 2024

⚪️ *Waziri wa Madini – Mhe. Anthony Mavunde*

✔️Jukwaa la kutangaza madini ya vito: Mnada huu ni sehemu muhimu ya kuonyesha thamani ya madini ya vito nchini, hususan Tanzanite, na fursa zake kiuchumi.

✔️Kufungamanisha sekta za kijamii na kiuchumi: Kupitia minada hii, tunaifanya Sekta ya madini kuwa kiunganishi kwa maendeleo ya jamii na sekta nyingine kama viwanda na utalii.

✔️Kuimarisha sekta ya madini: Minada ya madini ni kichocheo cha ukuaji wa sekta hii kupitia uwazi na ushindani wa soko.

✔️Uendelevu wa minada: Serikali imejipanga kuhakikisha minada hii ya madini ya vito inaendelea kufanyika mara kwa mara hapa Mirerani.

✔️Uhakika wa usimamizi wa madini yaliyobaki: Madini ambayo hayatauziwa mnadani hayatachukuliwa na Serikali bali yatarejeshwa kwa wahusika. Aidha, yale yaliyohifadhiwa Benki Kuu yatashughulikiwa.

✔️Maendeleo ya wachimbaji wadogo: Minada ya wachimbaji wadogo (brokers) itaendelea kufanyika na mnada mwingine wa aina hiyo umepangwa kabla ya mwisho wa mwezi huu.

✔️Mipango ya uwekezaji: Niwahimize Wakuu wa Mikoa kutenga maeneo maalum kwa uwekezaji wa madini. Mfano kwa mkoa huu wa Manyara, tunaendelea na mazungumzo tutaenda kujenga Tanzanite Smart City ambako litakuwa na ukumbi mkubwa wa mikutano na kuwa kitovu cha mikutano ya kimataifa na utalii.

⚪️ *Mkuu wa Mkoa wa Manyara – Mhe. Queen Cuthbert Sendiga*

✔️Fahari ya mkoa: Manyara inaonyesha umaarufu wake kama makazi ya madini adimu ya Tanzanite.

✔️Kuongeza pato la Serikali: Minada ya madini ya vito ni fursa ya kuongeza mapato ya Serikali sambamba na kutangaza utajiri wa mkoa.

✔️Tanzanite Rally: Hii ni sehemu ya juhudi za kutangaza Tanzanite na kukuza utalii wa madini kupitia matukio makubwa ikiwemo hizi mbio za magari tuliyoamua kuipa jina la madini yetu ya kipekee ya Tanzanite.

⚪️ *Naibu Katibu wa Wizara ya Madini – Msafiri Mbibo*

✔️Kurejeshwa kwa minada: Serikali imeanzisha minada ya ndani ili kuongeza ushindani na uwazi katika soko la madini ya vito wakati tukijiandaa kuelekea masoko ya kimataifa siku za usoni yatayofanyika hapa hapa.

✔️Kuwavutia wanunuzi wa ndani na nje: Ushindani na uwazi utasaidia kuvutia wanunuzi wa kimataifa, hivyo kuongeza thamani ya madini yetu.

✔️Washiriki wa mnada: Mnada huu umevutia jumla ya washiriki 195 wakiwemo wafanyabiashara wadogo 120, wakubwa 59, wachongaji madini 7, na wachimbaji 9.

✔️Thamani ya madini yanayouzwa: Madini yaliyopo mnadani yamekadiriwa kuwa na thamani ya shilingi bilioni 3.1.

✔️Kiasi cha Madini: Uzito wa madini yanyayofanyiwa mnada leo ni jumla ya kilogram 184.06.

⚪️ *Mwenyekiti wa Tume ya Madini – Janet Lekashingo*

✔️Usimamizi wa madini: Minada inalenga kuboresha uwazi na usimamizi wa biashara ya madini ya vito.

✔️Kuhamasisha wanunuzi: Wanunuzi wasiofanikiwa wanahimizwa kutokata tamaa kwani fursa zaidi zitakuja katika minada ijayo.

✔️Madini yanayouzwa: Aina ya ya vito yanayouzwa leo mnadani ni pamoja na Tanzanite, sphire, spinel, tourmaline

⚪️ *Mbunge wa Jimbo la Simanjiro – Mhe. Christopher Ole Sendeka*

✔️Kutekeleza ahadi: Amepongeza Waziri wa Madini kwa utendaji wake wa dhati katika kutimiza ahadi alizozitoa.

✔️Benki Kuu kununua dhahabu: Ameelezea hatua hii kuwa ni maono makubwa kwa uchumi wa nchi.

✔️Vision 2030: Madini ni Maisha na Utajiri: Sekta ya madini inalenga kufanikisha utafiti wa kina wa madini (airbone geophysical survey) kwa angalau asilimia 50 kufikia mwaka 2030, ikiwa ni hatua ya kuimarisha uchumi wa taifa.


⚪️ *Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Manyara – Mhe. Peter Toima*

✔️Maendeleo ya sekta ya madini: Chama kimeridhishwa na maendeleo ya sekta hii, hususan kwenye mkoa wa Manyara.

✔️Kuboresha maisha ya wananchi: Minada ina nafasi kubwa ya kuboresha maisha ya wakazi wa Mirerani na uchumi wa mkoa mzima kwa ujumla.

✔️Mwendelezo la minada: Chama cha Mapinduzi (CCM) kinasisitiza umuhimu wa kuhakikisha minada hii inakuwa endelevu.


⚪️ *Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini – Mhe. Kilumbe Shaban Ng’enda*

✔️Kuongeza bajeti ya Wizara ya Madini: Kamati imehimiza ongezeko la bajeti kwa ajili ya kufanikisha shughuli za utafiti na maendeleo ya sekta ya madini.

✔️Uwazi katika minada: Mnada huu ni ushuhuda wa uwazi katika shughuli za sekta ya madini.

✔️Usimamizi wa sekta kwa vizazi vijavyo: Bunge litaendelea kuhakikisha sekta ya madini inafaidisha vizazi vya sasa na vijavyo kupitia usimamizi bora.

http://BAADHI YA DONDOO ZA VIONGOZI WALIOZUNGUMZA KATIKA HAFLA YA UZINDUZI WA MNADA WA KWANZA WA MADINI YA VITO, MIRERANI – DESEMBA 14, 2024

Previous articleSTAMICO KUANZA USAMBAZAJI WA NISHATI SAFI YA RAFIKI BRIQUETTES ZANZIBAR
Next articleGAVANA BWANKU AENDELEA KUGAWA MIPIRA KWA TIMU MBALIMBALI NDANI YA TARAFA YA KATERERO.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here