Home LOCAL ELIMU YA HATIFUNGANI YA MIUNDOMBINU YA BARABARA (SAMIA INFRASTRUCTURE BOND) YATOLEWA JIJINI...

ELIMU YA HATIFUNGANI YA MIUNDOMBINU YA BARABARA (SAMIA INFRASTRUCTURE BOND) YATOLEWA JIJINI MWANZA

Mwanza

Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) na Benki ya CRDB wameendelea kutoa elimu kuhusu Hatifungani ya Miundombinu ya Barabara za Wilaya (Samia Infrastructure Bond) kwa wadau mbalimbali mkoani Mwanza.

Elimu hiyo imetolewa leo tarehe 06 Desemba, 2024 katika ukumbi wa Rock City Mall mkoani Mwanza.

Akitoa salamu za TARURA, Meneja wa TARURA Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Makori Kisare amesema wao kama wasimamizi wa ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya barabara za wilaya wamefurahi sana kwa kuanzishwa kwa Hatifungani ya Miundombinu ya Barabara (Samia Infrastructure Bond)
iliyozinduliwa rasmi na kwa mafanikio makubwa na Makamu wa Rais, Mhe. Dkt Philip Mpango tarehe 29/11/2024 jijijini Dar es Salaam.

“Sisi kama wanufaika wakubwa tumefurahi sana kwa kuanzishwa kwa hatifungani hii itakuwa ni miongoni mwa suluhisho kwa wakandarasi wetu hasa wazawa kupata fedha za kutosha ambazo zitawawezesha kutekeleza miradi kwa ufanisi na kulipwa kwa wakati kulingana na mikataba”.

Amesema wazo la kuanzishwa kwa hatifungani hii lilitoka kwa Waziri wa Nchi, OR-TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kutafuta njia sahihi ya kugharamia miundombinu inayosimamiwa na TARURA.

“Kipekee napenda kumpongeza na kumshukuru sana Mhe. Rais kwa maagizo yake ambayo Mhe. Waziri aliyasimamia na sisi TARURA tumeyatekeleza”, Amesema.

Aidha, Mhandisi Makori amewaomba wawekezaji mbalimbali ambao sio wakandarasi walio tayari kuwekeza katika hatifungani hiyo wasisite kuuliza maswali ili waweze kuelewa zaidi kuhusu hatifungani hiyo ili wanapowekeza wajihakikishie wanawekeza sehemu salama ambapo pia amewahakikishia kwamba hatifungani hiyo ni sehemu salama ya kuwekeza.

Hatifungani ya Miundombinu ya Barabara za Wilaya (Samia Infrastructure Bond) ni fursa nzuri ya uwekezaji kwa Watanzania ambapo moja ya faida zitokanazo na uwekezaji wake ni riba ya asilimia 12 kwa kila mwaka kwa miaka mitano.

http://ELIMU YA HATIFUNGANI YA MIUNDOMBINU YA BARABARA (SAMIA INFRASTRUCTURE BOND) YATOLEWA JIJINI MWANZA

Previous articleSERIKALI BEGA KWA BEGA NA WAFANYABIASHARA KUTATUA CHANGAMOTO ZAO
Next articleKINONDONI YAZINDUA KAMPENI YA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA,YATAJA WALIOFUNGWA MAISHA KWA MAKOSA YA UKATILI.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here