Viongozi mbalimbali akiwemo Spika wa Bunge la Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Naibu Spika la Tanzania Mussa Azzan Zungu, Mawaziri wakuu pamoja na Manaibu Waziri wamewasili katika viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni hayati Dkt. Faustine Ndugulile.
Spika Tulia akijadiliana jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), William Lukuvi.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda akiwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega.
Naibu Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu akisalimiana na mmoja wa viongozi.
Naibu Waziri wa TAMISEMI, Zainab Katimba (kulia) akijadiliana jambo na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa pamoja na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Ulega.