Mkuu wa Wilaya ya ILALA Edward Mpogolo amewaongoza wananchi wa Wilaya hiyo kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za mitaa unaofanyika leo nchi mzima Tanzania Bara.
Akizungumza mara baada ya kupiga kura yake katika Mtaa wa Karume Kata ya Ilala, Mpogolo amesema kuwa hali ya utulivu na amani imeendelea kutamaraki katika maeneo yote ya wilaya ya ilala.
Amesema wanayo mitaa 159 ambayo inaendelea na uchaguzi na zaidi vituo 2496 ambapo hali ni nzuri katika vutuo vyote na vifaa vinafanya kazi vizuri.
Aidha, DC Mpogolo amewahimiza wananchi kuendelea kujitokeza kupiga kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, huku akisema ulinzi na usalama umeimarishwa kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika salama.
Mpogolo, amepiga kura katika Kituo Namba moja, Mtaa wa Karume, Jijini Dar es Salaam na kuwashukuru wananchi kuwa na utukivu.
“Utulivu umeimarika, hali ya vifaa vya kupigia na usalama viko iko vizuri. Wananchi wameitikia wito wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan. Idadi ya watu waliojitokeza ni kubwa,” amesema.
“Wanaotaka kufanya vurugu waache kupanga mikakakati hiyo kwa sababu jeshi la polisi limejiandaa kikamilifu.”ameeleza.
Aidha aliwataka wananchi wanapomaliza kupiga kura kuondoka katika vituo hivyo kuendelea na majukumu mengine ya kulijenga taifa.