Home BUSINESS MILIONI 455 KUSAMBAZA MITUNGI YA GESI 22,00

MILIONI 455 KUSAMBAZA MITUNGI YA GESI 22,00

Tabora

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umetoa kiasi cha shilingi milioni 455.7 kwa ajili ya kusambaza mitungi ya gesi ipatayo 22,785 mkoani Tabora ukiwa na lengo la kuhamasisha na kuchochea matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini.

Hayo yamebainishwa leo Novemba 22, 2024 na Mkurugenzi wa Teknolojia za Nishati Jadidifu na Mbadala, Mha. Advera Mwijaje wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi ya REA ya mkoani humo.

Amezitaja wilaya zitakazonufaika kuwa ni pamoja na Wilaya ya Uyui, Urambo, Nzega, Sikonge, Kaliua, Igunga na Wilaya ya Tabora.

Kwa upande wake, Katibu Tawala Mkoa wa Tabora, Dkt. John Mboya amesema kuwa, suala la Nishati Safi ya Kupikia sasa ni ajenda ya kimataifa na wataibeba katika kuelimisha umma kuhusu matumizi salama ya nishati hiyo kwa upana.

Dkt. Mboya ameipongeza REA kwa mradi huo na miradi mingine mbalimbali inayoendelea kutekelezwa mkoani humo ikiwemo ya kufikisha umeme kwenye vijiji na vitongoji.

“Nawapongeza REA kwa kuendelea kusambaza mitungi ya gesi ili kuhamasisha matumizi ya nishati safi. Nawapongeza pia kwa kuendelea kufikisha umeme katika maeneo mbalimbali, natoa rai kwenu kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali yakiwemo makampuni makubwa katika kutekeleza miradi hiyo nchini ili kuifanya kuwa na tija kwa wananchi.” Amemalizia Dkt. Mboya.

Previous articleTUTAENDELEA KUSHIRIKIANA NA WADAU KATIKA KUIMARISHA SEKTA YA AFYA NCHINI – MAJALIWA
Next articleMNEC ASSAS AELEZA MKAKATI WA CCM KATIKA VITUO 87,000 VYA KUPIGA KURA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here