Home LOCAL BALOZI WA PAMBA TANZANIA AWASILI WILAYANI MAGU KUHAMASISHA KILIMO BORA CHA ZAO...

BALOZI WA PAMBA TANZANIA AWASILI WILAYANI MAGU KUHAMASISHA KILIMO BORA CHA ZAO LA PAMBA

Balozi wa Pamba nchini Tanzania, Agrey Mwanri leo Jumanne Novemba 19, 2024 amewasili Wilayani Magu kwa ajili ya kufanya uhamasishaji wa kilimo bora cha zao la pamba Wilayani humo.

Balozi Mwanri alipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Magu Mhe. Joshua Nassari na kufanya mazungumzo katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya.

Akizungumza na Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi mtendaji na watumishi wa idara ya kilimo balozi Mwanri amesema kuna haja ya kuongeza nguvu ya kutoa elimu kwa Wakulima wa zao hilo ili kuepukana na changamoto ya wakulima kulima kiholela ambapo husababisha kuvuna nje ya matarajio.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Magu Mhe. Joshua Nassari ameahidi kutoa ushirikiano kwa balozi wa pamba katika zoezi hilo ili kuongeza tija ya uzalishaji wa zao la pamba.

Uhamasishaji wa kilimo bora cha zao la pamba utaambata na shughuli ya utoaji wa elimu na kungoa na kuchoma moto masalia ya pamba na kupalilia kwaajili ya kuanza kupanda.

Previous articleCCM YASAMBAZA VIONGOZI NA MAKADA WAANDAMIZI NCHI NZIMA
Next articleWIZARA YA MADINI KUSIMAMIA VYAMA VYA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI,KASSIM MAJALIWA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here