Home LOCAL TUTASIMAMA NA WAKUNGA KUHAKIKISHA UZAZI UNAKUWA BARAKA, FURAHA TANZANIA – DK GWAJIMA.

TUTASIMAMA NA WAKUNGA KUHAKIKISHA UZAZI UNAKUWA BARAKA, FURAHA TANZANIA – DK GWAJIMA.

Na:Catherine Sungura.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima amewahakikishia wakunga kwamba Serikali itaendelea kusimama nao vema ili waweze kutimiza majukumu yao ipasavyo katika kusimamia akina mama kujifungua salama.

Dk. Gwajima ametoa pongezi hizo mapema leo alipozungumza kupitia kipindi cha Good Morning kinachorushwa na Kituo cha Radio cha Wasafi FM, kilichokuwa na mada kuhusu Siku ya Wakunga Duniani ambayo hufanyika Mei 5, kila mwaka.

Amewapongeza wakunga na wadau wote waliofanikisha maadhimisho ya siku hiyo nchini hususan UNFPA (Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Masuala ya Idadi ya Watu).

“UNFPA wametuunga mkono siku zote kuhakikisha tunakwenda vizuri na agenda hii ambayo wao wanaisimamia vema kuhusu idadi ya watu duniani  na maisha bora ikiwemo masuala ya afya.

“Siku ya leo tutakuwa tunaelekeza nguvu nyingi kuangalia vipaumbele vyote vya Umoja wa Mataifa (UN) na malengo yake 17 (SDGs), lengo namba tatu linahusu watu wa afya na ustawi wa jamii yetu tunavyoihudumia.

Ameongeza “Wakunga wanafahamu siku ya leo kauli mbiu inaeleza tuongozwe na takwimu maana ndiyo eneo muhimu litatufanya tuweze kujipima kama tutafika hayo malengo ya 2030.

“Katika malengo haya ambayo tumejiwekea kwamba vifo vya uzazi vitokomezwe kabisa, isifikie kwamba mama anabeba ujauzito anakwenda kujifungua anapoteza maisha au mtoto anapoteza maisha.

“Mchezo huu unawahitaji wakunga, wao ndiyo Baraka ya kwanza kabisa ya kiumbe hai ambacho mungu amekileta duniani, nini jukumu letu tunatakiwa tuwasaidie, tuwajali, tuwaenzi, wawe na imani.

“Kwa sababu kama wakirudi nyuma kwenye hotuba ya Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Nchi, Samia Suluhu Hassan, alipokuja bungeni alisema kwamba mradi huu wa masuala ya kuboresha huduma za uzazi wajawazito, wazazi na watoto wasifariki ni mradi wake wa moyoni.

“Kama Rais amesema ni mradi wa moyoni na ameniamini mimi na kunipa dhamana kusimamia sekta hii mimi ndiyo nazama kabisa moyoni mwake kabisa mzima mzima,” amesisitiza.

Dk. Gwajima ameongeza “Kwa hiyo naunga na mheshimiwa Rais. kwamba na mimi mradi huu ni wa moyoni mwangu na nitahakikisha nasimama na wakunga.

“Kuhakikisha kwamba tunawekeza kuwahakikishia wana uwezo wa kitaaluma mahitaji, miundombinu wanayohitaji, dawa zote na wanafanya kazi zao vizuri kuhakikisha wanakuwa Baraka kwa mtoto huyu anayezaliwa mikononi mwao, wao wakiwa wanafungua njia ya maisha bora yenye afya na furaha kwa mtoto huyu ambaye ni Taifa la kesho,” amesema Dk. Gwajima.

MWISHO

Previous articleKAMPUNI YA SEMS APPAREL KUGUSA WENYE MAHITAJI
Next articleVIDEO: DKT. GWAJIMA KUWANYOOSHA WAUZA DAWA BANDIA ZA BINADAMU “NI SAWA NA MAGAIDI”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here