DAR ES SALAAM.
MBUNIFU nguli wa mavazi nchin, Martin Kadinda ameibuka kinara wa tuzo za Harusi msimu wa kwanza kwa upande wa mavazi ya kiume.
Tuzo za Harusi kwa mara ya kwanza zimefanyika juzi katika hoteli ya Serena zilihusisha watoa huduma mbalimbali katika sekta ya harusi.
Akizungumza na wandishi wa habari Kadinda amesema amefurahishwa na ushindi huo na kuwapongeza waandaaji wa tuzo hizo kwa utaratibu wao.
“Nimefurahi kupata tuzo hii na na shukuru wote walio nipigia kura pia mchakato mzima wa kuchagua na kupiga kura kwa washiriki ulikuwa wa wazi, “ alisema Kadinda.
Aliongeza kuwa washiriki wenzake walikuwa wazuri ila wamezidiana hamasa na uwezo katika kazi hivyo atazidi kuwa mbunifu katika kazi zake ili kuendelea kuwa katika ubora wa juu.
Hii ni mara ya tisa kwa Martin kadinda kutwaa tuzo ya mbunifu bora wa mavazi ya kiume katika matamasha tofauti ndani na nje ya nchi.