Home FASHIONS KADINDA ANG’ARA TUZO ZA HARUSI.

KADINDA ANG’ARA TUZO ZA HARUSI.

 

DAR ES SALAAM.

MBUNIFU nguli wa mavazi nchin, Martin Kadinda ameibuka kinara wa tuzo za Harusi msimu wa kwanza  kwa upande wa mavazi ya kiume. 

Tuzo za Harusi kwa mara ya kwanza  zimefanyika juzi katika hoteli ya Serena zilihusisha watoa huduma mbalimbali katika sekta ya harusi.

Akizungumza na wandishi wa habari  Kadinda amesema amefurahishwa na ushindi huo na kuwapongeza waandaaji wa tuzo hizo kwa utaratibu wao.

“Nimefurahi kupata tuzo hii na na shukuru wote walio nipigia kura pia mchakato mzima wa kuchagua na kupiga kura kwa washiriki  ulikuwa wa wazi, “ alisema Kadinda.

Aliongeza kuwa washiriki wenzake walikuwa wazuri ila wamezidiana  hamasa na uwezo katika kazi hivyo atazidi kuwa mbunifu katika kazi zake ili kuendelea kuwa katika ubora wa juu.

Hii ni mara ya tisa kwa Martin kadinda kutwaa tuzo ya mbunifu bora wa mavazi ya kiume katika matamasha tofauti ndani na nje ya nchi.

Previous articlePUBLIC NOTICE: DISIGNATION OF TMDA AS REGULATOR OF TOBACCO PRODUCTS.
Next articlePROF. MAKUBI AHIMIZA UFANISI UPIMAJI COVID 19 UWANJA WA NDEGE WA JULIUS NYERERE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here