WAZIRI Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe:Mohamed Mchengerwa akiongea na makatibu mahususi katika mkutano wao uliofanyika Arusha. |
Mwenyekiti wa TAPSEA Bi Zuhura Songambele Maganga akizungumza katika mkutano wao wa 6 Mkoani Arusha. |
NA: NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
waziri ofisi ya rais menejimenti ya utumishi mma utawala bora Mhe:Mohamed Mchengerwa amesema kuwa kada ya makatibu mahususi ni kada ni kada muhimu ambayo serikali wanaitegemea katika kutimiza majukumu yake ya kila siku hivyo wanawajibu wa kuwajibika ipasavyo.
Sambamba na hayo pia amemuagiza katibu mkuu wa wizara hiyo kupelekea kazi data ya makatibu mahususi ili kusaidia kujua kila mmoja atapelekwa wapi na atasaidia nini kwani wao ndio sura na taswira ya ofisi yoyote.
Mchengerwa aliyasema hayo wakati akifungua mkutano mkuu wa 6 wa sita wa chama cha makatibu mahususi (TAPSEA)uliofanyika mkoani Arusha na kukutanisha makatibu 2900 kutoka mikoa mbalimbali ambapo aliwataka wafanye kazi kwa weledi na uzalendo hasa kulingana na umuhimu wa kada yao.
Alieleza kuwa makatibu mahususi wanamajukumu mengi ikiwemo kutunza vifaa vya ofisi pamoja na kutunza siri hivyo wana wajibu wa kubadilika na kuendeleza moyo wa uchapakazi kwani hataki kusikia makatibu hao waashikiliwa na TAKUKURU kwa kishindwa kuwa waaminifu.
“Mnapoona mtu haendi vizuri toeni taarifa kwani kwasasa hakutakuwa na umiliki wa kuajiriwa sehemu fulani tutawatoa kama ufanisi wenu sio mzuri hivyo kila mmoja achape kazi na lazima awajibike,” Alisema Mhe Mchengerwa.
Aidha alisema kiwa wizara imetenga bajeti ya shilingi bilioni 243 ili kuhakikisha kwamba watumishi wanapandishwa madaraja ambapo pia amemuagiza katibu mkuu wa wizara hiyo kumuandalia kikao na maafisa utumishi wote nchini ili kutatua changamoto ya iliyopo kati ya watumishi na maafisa hao linapokuja suala la upandishaji wa vyeo.
Kwa upande wake katibu mkuu ofisi ya Rais menejiment ya utumishi na utawala bora Laurent Ndumbaro alisema kuwa mambo mengi yanawategemea makatibu mahususi kwasababu yaapita kwao hivyo watunze siri za ofisi wanazozijua kwa nafasi zao.
Naye mwenyekiti wa TAPSEA Zuhura Songambele Maganga alisema kuwa katika mkutano huo wameweza kufundishwa mada mbalimbali ikiwemo usalama wa ofisi na utinzaji wa siri za ofisi pamoja na udhibiti wa hisia na migogoro sehemu za kazi.
Bi Maganga alieleza kiwa lengo ni kuendelea kuwapiga msasa na kuboresha kazi za makatibu hao ambapo wamefanikiwa kuwakutanisha bara na visiwani pomoja na kuongeza thamani ya kada hiyo kwa kuwa na elimu ya juu.
Alisema pamoja na mafanikio hayo bado wanakabiliwa na changamoto baadhi ya waajiri kutokutambua umuhimu wa kada hiyo na kukosa fursa mbalimbali ikiwemo mafunzo ya muda mfupi na muda mrefu ambapo pia alisema waajiri wengine kutowataka katika ofisi zao makatibu mahususi ambao umri umeenda.
Pia aliiomba serikali kusimamia ngazi ya uhadhiri kataka kada hiyo, kurudisha TPS 6 bora bila kushirikisha kada zingine pamoja na kuendelea kulinda maslahi ya makatibu mahususi.