(Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW).
Na:Mwandishi Wetu, DODOMA.
Wazee wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhassan kwa kusimamia na kuboresha huduma ya matibabu kwa Wazee katika Hospitali mbalimbali nchini.
Shukrani hizo zimetolewa kwa nyakati tofauti na wazee wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii, Mwanaidi Ali Khamis katika hospitali ya Benjamin Mkapa iliyopo jijini Dodoma kujionea utekelezaji wa maelekezo yaliyotolewa juu ya kuboresha huduma za matibabu kwa wazee.
Mzee Anthony Mwakyusa aliyekutwa dirisha la dawa amesema kwa hivi sasa naona huduma zimekuwa nzuri zaidi hasa kwa sisi wazee wanahudumiwa harakaharaka na Madktari wanasikiliza shida zao na wanawahudumia vizuri sana.
Ameongeza kuwa wanawashukuru sana kwakwa viongozi wa kitaifa kufuatilia jinsi wazee wanavyohudumiwa kiukweli huduma zimekuwa bora sana.
Kwa upande Mzee Hassan Kijuu amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwaona wazee kuwa ni kundi maalum na linalohitaji kuangaliwa zaidia katika kupatiwa huduma mabaliambali hasa huduma za afya.
“Nimefika kwenye foleni na namba yangu ilikuwa mbali sana lakini alikuja binti simjui, hanijui akaniomba karatasi zangu mara nimepelekwa huku, mara nimepelekwa kule na sasa nimemaliza, tunawashkuru sana.” alisema Mzee Kijuu.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii, Mwanaidi Ali Khamis ameipongeza Hospitali ya Benjamin Mkapa kwa huduma bora kwa wazee na kuwapongeza madakatari na Maafisa Ustawi wa Jamii kwa huduma zao nzuri wanazotoa kwawazee hao.
“Niwashukuru madaktari wa Hospitali hiyo pamoja na Maafisa Ustawi wa Jamii kwa kuwaangalia vyema wazee hao na naviagiza vituo vyote vya kutolewqa huduma za afya pamoja na Hospitali zote nchini kuendelea kutekeleza agizo hili” alisema Naibu Waziri Mwanaidi.
Aidha Naibu Waziri Mwanaidi amewahakikishia wazee kuendelea kuoata huduma bira na kwa wakati na kuwaomba waendelee kuishauri Serikali pale panapokuwa na mapungufu ili waendelee kuboresha huduma mbalimbali katika kutoa huduma bora za afya.
Pia Naibu Waziri Mwanaidi amipongeza Hospitali ya Benjamini Mkapa hospitali hiyo kwa ubunifu wake wa kutenga eneo la kupumzikia wazee likiwa na viburudisho mbalimbali kama chai na kahawa pamoja na runinga na kuzitaka hospitali zingine kuiga ubunifu huo wa kuboresha zaidi ya kutoa huduma kwa wazee.
“Wazee ni tunu katika nchi yetu. Wameijenga nchi yetu katika vipindi tofauti na sisi kama wizara tutahakikisha wanapata huduma bora zaidi za matibabu. Nimefurahishwa sana na namna madaktari pamoja na maafisa ustawi wa jamii wanavyowahudumia wazee katika hospitali hii.” Alisema Naibu Waziri Mwanaidi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dkt. Alphonce Chandika amesema Hospitali yake imepokea maelekezo hayo na wameshaanza kuyatekeleza na wamejipanga kuwahudumia wazee wa rika tofauti wakiwemo wenye uoni hafifu na hivyo waratibu wa wazee huwafuata wazee mara wafikapo hospitalini na kuwaongoza kwenye kupata huduma.
“Kila eneo la kutolea huduma tumeweka mtumishi ambaye atashughulikia huduma za wazee na kuhakikisha wanapata matibabu kwa wakati, lakini pia kuhakikisha kama anatakiwa kwenda sehemu nyingine kupata huduma kama maabara, huyo mtumishi atatakiwa kuhakikisha anamfikisha mzee sehemu husika ya huduma,” alifafanua Dkt. Chandika.
Mnamo tarehe 7 Mei, mwaka huu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati akiongea na wazee wa Mkoa wa Dar es salaam aliahidi kuboresha tiba kwa wazee kwani tiba ni haki yao ya msingi katika daraja lolote lile watakalokua wanaugua kuanzia vituo vya afya, Zahanati hata hospitali za Taifa.
MWISHO