Home ENTERTAINMENTS BSS YAZINDULIWA ,SASA NI BONGO STAR SEARCH AFRIKA

BSS YAZINDULIWA ,SASA NI BONGO STAR SEARCH AFRIKA

SHINDANO la kusaka Vipaji Tanzania Bongo Star Search ‘BSS’ misimu wa kumi na tano umezinduliwa rasmi kwa sasa ni Bongo Star Search African wataenda kimataifa Kenya, Uganda na Congo.

Akizungumza na wakati wa uzinduzi wa misimu huo mpya Mkurugenzi Mkuu wa Benchmark 360 Limited Rita Paulsen amesema kuwa Msimu huu wa kumi na tano wa Bongo Star Search ni wa kipekee sana, na ni wa kihistoria.

“Kwanza kabisa, napenda kuchukua fursa hii kumshukuru Mungu na kuwashukuru wote
mliojitokeza kwa wingi kushuhudia tukio hii kubwa, uzinduzi wa msimu mpya wa Bongo Star Search Afrika.

“Kwa miaka mingi tumeweza kuibua vipaji kutoka Tanzania pekee, lakini msimu huu tunaingia hatua ya juu kabisa. Kwa mara ya kwanza, tunavuka mipaka ya nchi, tukifanya usahiri katika nchi zaidi ya tano, zikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi, na Congo.

“Lengo letu kuu ni kufungua fursa kwa vijana wengi zaidi kutoka ukanda mzima wa Afrika Mashariki na Kati, kuwapa jukwaa la kuonesha vipaji vyao na kuendeleza ndoto zao.”amesema Madam Ritha

Amesema kuwa “Muziki ni lugha ya ulimwengu, na tunataka kuwapa wasanii chipukizi kutoka sehemu mbalimbali nafasi ya kuungana na kuunguruma kwenye jukwaa hili kubwa.

“Msimu huu, kama mlivyosikia, utakua ni mkubwa zaidi kuwahi kutokea.Tumeweka mipango madhubuti kuhakikisha kuwa sio tu tunaboresha uzoefu wa mashindano, lakini pia tunapandisha kiwango cha ubora katika kila hatua.

“Tutakuwa na majaji wa kimataifa, waelimishaji wenye uzoefu, na wasanii waliobobea watakaoshirikiana na washiriki wetu ili kuhakikisha kuwa wanapata elimu ya juu na mwongozo sahihi wa kimasoko na kisanii.

Kwa upande wake Meneja Masoko wa Sartimes David Malisa amesema kuwa Bongo Star Search wanasheherekea miaka kumi na tano tangu kuanzishwa kwake na mwaka huu wamevuka kimataifa zaidi.

“Kama mlivyosikia wataenda nchini Kenya Uganda pamoja na Congo sio kitu kidogo wamepiga hatua sana ni jambo la kuwapongeza.Lakini Bongo Star Search itaanza kuonyeshwa Desemba 1 kupitia chanel ya ST bongo kwa hapa Tanzania wakati Uganda Star Times Makula tv wakati Nairobi St Swahili chanel 160 & 400.”amesema Malisa

Previous articleMKUTANO WA PILI WA BRELA NA WADAU, NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA ASISITIZA MIFUMO ISOMANE 
Next articleZIARA YA WAZIRI KIJAJI KATIKA WILAYA YA PANGANI, TANGA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here