Na: Mwandishi WETU
KIKOSI cha Tanzania Prisons leo wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya vigogo, Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Bao pekee la Tanzania Prisons limefungwa na Nahodha wake, Benjamin Asukile dakika ya 54 na kwa ushindi huo, wanafikisha pointi 29 za mechi 29 na kusogea nafasi ya 14.
Kwa upande wao, Simba wanabaki na pointi zake 60 nafasi ya pili nyuma ya mabingwa tayari, Yanga wenye pointi 71 baada ya wote kucheza mechi 29.