Maafisa wa Kampuni ya CO_PACKAGES ya Jijini Dar es Salaam Asimwe Godfrey (kushoto) na Cherie Ngayahika (kulia) wakionesha Bidhaa wanazozalisha na kuziuza wakiwa kwenye Banda lao katika maonesho hayo. |
Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM.
Mjasiriamali na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya CO_PACKAGES ya Jijini Dar es Salaam inayojishughulisha na utengenezaji wa kazi mbalimbali za mikono Evaglory Lwebangira amesema kuwa jamii ya watanzania kwa kiasi kikubwa imehamasika na kuanza kuthamini na kutumia bidhaa zinazotengenezwa na wajasiriamali wa hapa nchini.
hayo ameyasema wakati wa mahojiano maalum yaliyofanyika kwenye maonesho ya wajasiriamali yajulikanayo kama IBUKE yanayofanyika kwa siku mbili katika viwanja vya Kijiji cha Makumbusho kilichopo Kijitonyama Dar es Salaam.
Lwebangira ambae amewahi kuwa mwalimu wa Ujasiriamali (Entrepreneurship) na Rasirimali watu (HR) katika chuo kimoja kilichopo Mkoani Kilimanjaro amebainisha kuwa wajasiriamali wengi wameweza kuzalisha vitu vizuri na vyenye ubora wa hali ya juu na hivyo kuifanya jamii ya Watanzania kuhamasika na kuanza uzitumia.
“kwa sasa Watanzania wamehamasika sana na kuanza kutumia bidhaa zetu hivyo imetupa hali ya kuongeza uzalishaji kwa kutengeneza bidhaa zenye ubora zaidi kwani soko lipo na bidhaa zinanunuliwa” amesema Lwebangira.
kwa upande wake moja ya mwanakamati wa maonesho hayo Rhoda Zablon amesema kuwa jumla ya wajasiriamali 40 wameshiriki kwenye maonesho hayo ya siku mbili na kwamba washiriki hao wametoka katika mkoa wa Dar es Salaam na mikoa mingine ya jirani ikiwemo Dodoma na Morogoro.
“Maonesho ni mazuri sana hapa tuna wajasriliamali wapatao 40 wanaoshiriki maonesho haya na bidhaa ni nzuri sana hivyo tunaamini watu mbalimbali wataendelea kufika hapa ili kujionea na kununua bidhaa zilizopo kutoka kwa wajasiriamali wetu” amesema Rhoda.
Maonesho hayo ya siku mbili yameandaliwa na umoja wa wanawake wajasiriamali na wafanyabiashara tofauti Tanzania. (BUSINESS GALA).