Na: Mwandishi wetu.
Leo tarehe 4 June Naibu waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Geofrey Kasekenya Ametembelea banda la STAMICO katika Maonesho ya wiki ya Mazingira yanayoendelea katika Viwanja vya Jakaya Kikwete.
Ameipongeza STAMICO kwa kubuni uzalishaji wa mkaa mbadala wa Makaa ya mawe ambao utakuwa ni mkombozi kwa wananchi na kwa mazingira.
Ameitaka STAMICO kutoa elimu na kuwashirikisha wananchi katika shughuli za Uchimbaji zinazoendelea katika Mgodi wa Makaa ya mawe-Kabulo uliopo Ileje-Songwe .