Home BUSINESS KAMISHNA JENERALI WA UHAMIAJI AVUTIWA NA NISHATI YA RAFIKI BRIQUETTES

KAMISHNA JENERALI WA UHAMIAJI AVUTIWA NA NISHATI YA RAFIKI BRIQUETTES

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji ((CGI) Dkt.Anna Makakala amevutiwa na nishati safi na salama ya kupikia ya Rafiki Briquettes inayozalishwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).

Aidha ametoa pongezi kwa uongozi wa STAMICO kwa wazo la kuwaweka wadau wake eneo moja kwenye Maonesho ya Madini yanayoendelea mkoani Geita.

Ametoa pongezi hizo leo tarehe 19 Oktoba wakati alipotembelea banda la STAMICO ambalo limepewa jina la “Kijiji cha STAMICO na Wadau Wake”.

Alivutiwa na nishati ya Rafiki Briquettes na kuahidi vyuo vya Uhamiaji nchini kuanza kuitumia.

“Naupongeza uongozi wa STAMICO kwa kuzalisha nishati hii ambayo itasaidia sana wananchi na hasa kina mama ambao wanataabika sana kwa moshi wa kuni na pia kuzitafuta mbali na maeneo yao wanayoishi”alisema na kuongeza:

“Nimefarijka kuona jinsi STAMICO ilivyowaleta pamoja wachimbaji wadogo,vikundi vya wanawake na wadau wengine kama vile watu wenye ualbino na wenye ulemavu wa kusikia”.

Mpangilio wa washiriki kwa bidhaa mbalimbali kwenye sekta ya madini pia umemvutia kiongozi huyo.

Vikundi ambavyo vimealikwa na STAMICO na kushiriki ndani ya banda moja ni pamoja na FEMATA,TAWOMA, TAMAVITA,FDH,Tanzania Youth Miners na Chama cha Wachimbaji Geita (GEREMA).

Wengine ni pamoja na kikundi cha Wanawake na Samia Geita na Chama cha Wanawake Geita (GEWOMA).

Baadhi ya wageni wengine mashuhuri waliotembelea Kijiji cha STAMICO leo ni pamoja na Mbunge wa Jimbo la Nyang’hwale Mkoani Geita,Mhe. Hussein Nassor Amar,Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhe.Martin Shigela na Katibu Tawala wa Wilaya ya Geita, Bi Lucy Beda

Viongozi hao wamepokelewa na Kaimu Meneja wa Masoko na Mahusiano wa STAMICO,Bw Gabriel Nderumaki ambae aliwapatia maelezo mafupi kuhusu ushiriki wa Shirika kwenye maonesho haya mwaka huu.

Amesema kuwa nishati ya Rafiki Briquettes ni mkombozi kwa Watanzania kutokana na kuuzwa kwa bei nafuu,rafiki kwa mazingira na afya.

Aidha,Bw Nderumaki amesema kuwa STAMICO inajivunia kufanya kazi na vikundi mbalimbali vya wachimbaji na kuongeza kuwa Shirika litaendelea kuvilea hivi vikundi.

 

Previous articleDC KINGARAME ATEMBELEA BANDA LA DIB MAONESHO YA MADINI GEITA
Next articleWAFANYAKAZI WA GEITA GOLD MINE WAONESHA NIA YA KUMILIKI NYUMBA KUPITIA NHC
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here