Home BUSINESS DKT. BITEKO ASISITIZIA UMUHIMU WA HIFADHI YA JAMII KWA WACHIMBAJI WADOGO

DKT. BITEKO ASISITIZIA UMUHIMU WA HIFADHI YA JAMII KWA WACHIMBAJI WADOGO

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dotto Biteko, ameonesha umuhimu wa hifadhi ya jamii kwa wachimbaji wadogo alipokuwa akitembelea banda la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) tarehe 5 Oktoba 2024, wakati wa Maonesho ya 7 ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea Geita.

Akiwa katika banda hilo, Mhe. Biteko alipokea maelezo kutoka kwa Bi. Lulu Mengele, Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma wa NSSF, aliyewasilisha kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba. Bi. Mengele alielezea jinsi Mfuko wa NSSF unavyowahudumia wachimbaji madini, ambao wengi wao ni wanachama wa Mfuko huo, na jinsi wanavyonufaika na huduma za kidijitali kupitia mfumo wa NSSF Portal.

Mfumo huu wa kisasa unawawezesha wanachama, waajiri, na wadau kufikia huduma mbalimbali, ikiwemo kuwasilisha michango, kupata taarifa za mchango, kufuatilia salio, na kufungua madai ya mafao kwa urahisi popote walipo. Bi. Mengele alisisitiza kuwa hii ni sehemu ya juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, kuhakikisha huduma za kijamii zinapatikana kwa ufanisi zaidi kupitia mifumo ya kidijitali.

Maonesho hayo ya Teknolojia ya Madini yamezinduliwa rasmi na Mhe. Dotto Biteko na yanaendelea hadi tarehe 13 Oktoba 2024, yakilenga kukuza uelewa wa teknolojia bora katika sekta ya madini.

Previous articleBoT YAWAKARIBISHA WACHIMBAJI KUUZA DHAHABU ZAO
Next articleS0MA MAGAZETI YA LEO OKTOBA 7- 2024
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here