DODOMA
BARAZA la Taifa la Mashirika yasiyo ya kiserikali (NaCoNGO) linatarajia kufanyaka uchaguzi wake kitaifa Julai 8, Mwaka huu jijini Dodoma kuweza kupata safu mpya ya viongozi watakaolisogeza mbele baraza hilo.
Akizungumzia uchaguzi huo jijni Dodoma mapema wiki hii Mwenyekiti wa Kamati ya uchagauzi wa NaCoNGO, Wakili Flaviana Charles, alibainisha kuwa tayari tathimini ya mwenendo wa uchaguzi wa baraza hilo ngazi ya wilaya ambapo amesema kuwa Juni 7, mwaka huu waziri Dkt. Gwajima alifanya uteuzi wa kamati ya mpito kwa ajili ya kuratibu na kusimamia uchaguzi wa Baraza la taifa la mashirika yasiyo ya kiserikali.
Wakili huyo amesema kuwa jukumu la kamati hiyo ni kuratibu na kusimamia uchaguzi wa Baraza hilo.
Amesema kuwa makundi hayo ni pamoja na mashirika ya kimataifa, watu wenye ulemavu pamoja na watoto na vijana.
“Kimsingi hii taarifa inalenga kutoa tathimini ya mwenendo wa uchagauzi wa Baraza la taifa la mashirika yasiyo ya kiserikali hususani ngazi ya wilaya uliofanyika Juni 26, mwaka huu “amesema.
Amesema kwa ujumla uchaguzi ulifanyika kwa amani na utulivu katika wilaya zaidi ya 130, za Tanzania bara ambapo kumekuwepo na mwitikio mkubwa na hamasa ya hali ya juu kwa wagombea na wapiga kura.
“Tathimini ya ujumla iliyofanyika katika wilaya zaidi ya 130, zilionyesha zoezi hilo kati ya watia nia watano waliochukua fomu za kuomba uongozi wa baraza jumla ya watia nia wanne walirudisha fomu kwa msingi huo mchakato wa wa kuchukua na kurudisha fomu ulifanikiwa kwa takribania asilimia 80”amesema.
“Ameongeza kuwa mchakatgo wa kupiga na kuhesabua kura ulifanyika juni 26, mwaka huu katika wilaya zote zilizopo ndani ya mikoa 25 ya Tanzania bara, isipokuwa katika wilaya za mkoa wa Kigoma.ambapo kwa upande wa Ruvuma ambako kulikuwa na changamoto kadhaa lakini watafanya uchaguzi wiki hii hivyo niwaoambe watu wa Ruvuma wajitokeze kwa wingi
Amesema baadhi ya wilaya uchaguzi haukufanyika kutokana na kukosekana wagombea wenye sifa waliojitokeza kuwania uongozi wa Baraza au wengine kupita bila kupingwa.
Aidha, kabla ya Julai 10, mwaka huu uchaguzi wa Baraza hilo kuanzia ngazi ya wilaya, mkoa hadi taifa utakuwa umekamilika na viongozi wapya kukabidhiwa rasmi ofisi
Hatua hiyo imekuja baada ya waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Dorothy Gwajima kutoa siku 30, kwa Baraza la Taifa la mashirika yasiyo ya kiserikali (NaCoNGO) kufanya uchaguzi ambapo Baraza litakaloundwa litakuwa na wajumbe 30, kati yao 26, kutoka katika mikoa yote ya Tanzania bara na wajumbe wanne watachaguliwa kutok.
Uchaguzi katika ngazi hii unasimamiwa na viongozi walioteuliwa na Kamati ya Uchaguzi ya Taifa. Wasajili wasaidizi ngazi wa mikoa watakuwa waangalizi huru wa uchaguzi katika mikoa husika.
Ifuatayo ni ratiba ya uchaguzi katika Mikoa.