Mkufunzi Mwandamizi kutoka Chuo cha Ualimu wa ufundi stadi (VETA) Morogoro Frank Ulio (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkufunzi kutoka katika Chuo hicho Sophia Tuka (wakwanza kulia) na Bellington Lyimo ambaye ni Mbunifu wa Vifaa vya Maabala VETA Morogoro (kulia). (PICHA NA: HUGHES DUGILO) |
Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM.
Wito umetolewa kwa wanafunzi wanaosomea masuala ya umeme kujitokeza kwa wingi kutembelea Banda la VETA katika Maonesho ya 45 ya Sabasaba ili kupata fursa ya kuona na kujifunza shughuli mbalimbali zinazotolewa na chuo cha uwalimu cha mafunzo ya ufundi stadi MVTTC.
Wito huo umetolewa na Mhandisi kutoka Frank Ulio kutoka katika chuo hicho alipokuwa akihojiwa na waandishi wa habari juu ya masuala mbalimbali ya namna chuo hicho kinavyotoa mafufunzo hayo na kusema kuwa wamekuja na kifaa maalum cha cha kufundishia ili kuweza kuwapa Elimu kwa ya kifaaa hicho kwani ni kifaa kipya na kitawasaidia kufikia malengo yao.
“Ndugu waandishi kikubwa kupitia maonyesho haya tunawaomba wanafunzi waje na wajitokeze kwa wingi ili waje kupata elimu stahiki kuhusu umeme na kama mnvyojua sisi ni chuo kwahiyo tupo hapa hadi julai 13 hivyo wajitokeze.”amesema Ulio.
Naye Mkufunzi mwandamizi wa Chuo hicho Sophia Tuka amezungumzia kozi mbalimbali zinatolewa na chuo hicho katika mwaka huu wa masomo nakusema kuwa chuo hicho kinatoa kozi mbalimbali za ualimu na kuwaandaa walimu wanofundisha ufundi.
“Wanahabari pia katika chuo chetu Tuna kozi ya postgraduetu ambayo imesajiliwa na TCU na tunashirikiana na nchuo kikuu huria na kimsingi tuna muhula wa mwezi wa tisa na nyingine itakuwa ya awamu ya pili “amesema.