Home LOCAL WAZIRI MKUU AMUWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA MKUTANO WA NANE WA OACPS

WAZIRI MKUU AMUWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA MKUTANO WA NANE WA OACPS

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Septemba 11, 2024 amemuwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Nane wa Mawaziri wa Umoja wa Nchi za Afrika, Karibian na Pasifiki (OACPS) wanaohusika na masuala ya Uvuvi, Bahari, Maziwa na Mito, kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Malengo ya mkutano huo ni kuimarisha utekelezaji wa Makubaliano yaliyofikiwa; kuimarisha utekelezaji wa vipaumbele vya kimkakati vya umoja; kubadilishana uzoefu; kuweka mikakati ya pamoja; na kuimarisha ushirikiano na washirika ili kuboresha usimamizi wa bahari, uchumi wa buluu, na maendeleo endelevu ya uvuvi.

Aidha, Mkutano huo unatarajiwa kutoa mwongozo wa kimkakati kwenye vikao vya juu vya maamuzi vya Umoja wa Nchi za Afrika, Karibian na Pasifiki ili kuboresha usimamizi wa bahari, uvuvi na ufugaji wa samaki endelevu.

Previous articleSOMA MAGAZETI YA LEO SEPTEMBA 11-2024
Next articleBASHE: MPINA CHEZEA SEKTA NYINGINE SIO KILIMO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here