Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM.
WANANCHI wameendelea kujitokeza Kwa wingi kwenye Banda la Chama cha wanawake wajasiliamali Tanzania (TWCC) ili kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na wajasiriamali na wafanybiashara kwa lengo la kutaka kujifunza masuala mbalimbali ya ujasaliamali.
Wananchi hao kupitia sikuku ya Sabasaba ambayo kila mwaka huadhimishwa Julai Saba wameonyesha kiu ya kutaka kujifunza na kutamani mafanikio ambayo tayari wengine wanayakata kutokana na kujikita kwenye ujasaliamali huo.
Akizungumza na waandishi wa habari mmoja wa Wananchi waliofika kwenye maonyesho hayo Sauli Willium amesema kuwa kabla ya kufika kwenye Banda hilo awali walizunguka sana kutafuta Banda la TWCC kwani kiu yao kubwa ilikuwa kufika kwenye Banda hilo ili kukutana na wajasiliamali na kupata uelewa zaidi
“Nimekuja na mke wangu ili tupate elimu ya ujasaliamali lakini pia tujifunze namna ya kutengeneza unga wa mihogo Kwa ajili ya lishe na tumepata uelewa wa kutosha sana.kuhusu utengenezaji wake na sasa tumekwenda kujipanga .” amesema William
Amefafanua kuwa TWCC ni chama cha Wanawake wajasiliamali nchini lakini hainamaana kuwa wakinababa hawana nafasi ya kufanya ujasariamali na kujiunga kwenye Chama hicho nakwamba ndio maana ameambatana na mke wake ili baada ya kumalizika maonesho ya Sabasaba waanze utengenezaji wa unga wa lishe kupitia zao la muhogo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TWCC Mwajuma Hamza akizungumzia ushiriki wao kwenye maonesho ya 45 ya Kimataifa amesema kuwa anawaomba Watanzania wa rika zote kusogea katika viwanja hivyo ambapo monesho yanaendelea hadi Julai 13 Mwaka huu.
Amesema wao kama TWCC wapo katika viwanja hivyo na Banda lao lipo karibu na jengo la Maliasili na Utalii na linabeba wajasiriamali wanawake kutoka Tanzania nzima hivyo na wanaonesho bidhaa mbalimbali za mikono na nyinginezo.
“Tunawakaribisha watu ambao wanataka kuwekeza na wanawake kwani kuina vitu vizuri hivyo waje kushirikiana katika biashara na kitu chatofauti ambacho wanaweza kukipata vipo vingi mno kikubwa waje kwa wingi hapa “amesema
Ameongeza kuwa maonesho yanamuamko mkubwa na mamlaka husika wamejitahdi kufanya maandalizi mazuri na nakwamba msimu huu ni tofauti na misimu mingine kwani mwaka huu watu wamekuwa wengi toka siku ya kwanza yalipoanza.