Na: Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM.
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,Hemed Abdullah anatarajia kuwa mgeni rasmi katika kufunga maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) alimaarufu sabasaba na kutoa tuzo kwa washindi wa zoezi la ukaguzi wa banda bora katika maonesho hayo.
Maonesho hayo yalianza rasmi Juni 18,2021 na kumalizika Julai 13,2021 jumla ya wageni 121 ambao ni viongozi wa Chama na Serikali, Mabalozi ,Wakuu wa Taasisi za Umma, Binafsi ,mashirika ya kimataifa pamoja na viongozi wa dini.
Akizungumza na Waandishi wa habari jana katika viwanja vya Sabasaba ,Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe alisema kipindi cha maonesho matukio kadhaa yenye kujenga kuongeza ufanisi katika sekta ya biashara waliweza kufanyika ikiwemo mikutano ya Biashara kwa njia ya mtandao ambayo ilianza kufanyika tangu juni 30 mwaka huu.
Alisema pia ndani ya maonesho hayo kulifanyika kwa uzinduzi wa tele la trekta lililotengenezwa na kampuni ya Kilimanjaro Machine Tools(KMTC) iliyo chini ya Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) ili kutangaza teknolojia ya kilimo inayotengezwa nchini uliofanyika Julai 6,2021.
“Uzinduzi wa mfumo wa taarifa za Biashara uliofanyika Julai 8,2021 ambapo lengo la kuanzishwa kwake ni kujenga na kuongeza uelewa kwa wafanyabiashara kufahamu taratibu za kufanya biashara ya kimataifa, “alisema.
Alisema Sambamba na maonesho hayo pia utekelezaji wa miongoni na tahadhari zote za kujikinga na ugonjwa wa UVIKO-19 zinazotolewa na wizara ya Afya zinatekelezwa ipasavyo kwa kushirikiana n Kamati maalum ya kitaifa ya masuala ya afya wakati wote wa maonesho hayo.
“Kupitia miongozo hiyo tumeweza kupunguza msongamano katika milango ya kuingilia kwa kuhamasisha watembeaji kukata tiketi kwa njia ya mtandao ,kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni ,kuweka vitakasa mikono katika maeneo mbalimbali ya uwanja na uhamasishaji wa uvaaji wa Barakoa,”alisema
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Temeke,Jocate Mwegelo alisema tangu maonesho yalivyoanza hadi leo hakuna
matukio ya uvunjifu wa amani yoyote yaliyotokea.
“Tumemaliza shughuli hii salama,hatujapata changamoto pia ya masuala ya usalama barabara, jeshi la polisi nalo limefanya kazi yake kubwa kwa kweli tunawashukuru wote waliofika katika maonesho haya, tuombe pia watu wajitokeze pia kwenye kufunga,”alisema
Mwisho