Home LOCAL MNADHIMU MKUU WA JWTZ AISHUKURU KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE ULINZI NA...

MNADHIMU MKUU WA JWTZ AISHUKURU KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE ULINZI NA MAMBO YA NJE YA SHELISHELI

Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Salum Haji Othuman ameishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge, Ulinzi na Mambo ya Nje ya Kisiwa cha Ushelisheli kwa kuthamini mchango mkubwa uliotolewa na JWTZ katika harakati za ukombozi barani Afrika.

Luteni Jenerali Othuman ameyasema hayo alipotembelewa na kamati hiyo Makao Makuu ya JWTZ Msalato jijiji Dodoma tarehe 03 Septemba 2024.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe Francois Adelaide amesema JWTZ limekuwa msaada mkubwa sana kwa nchi nyingi za kusini kwa Afrika.

Amesema nchi yake itaendelea kukuza diplomasia ya Ulinzi hasa kwenye mafunzo, mazoezi pamoja na kubadilishana ujuzi katika kukabiliana na uhalifu unaovuka mipaka pamoja na kukabiliana na majanga.

 

Previous articleTANZANIA KUJIIMARISHA ZAIDI KIDIPLOMASIA – MAJALIWA
Next articleNAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA MAENDELEO JAMII,JINSIA,WANAWAKE,NA MAKUNDI MAALUM AMEFUNGUA MAFUNZO YA SIKU MBILI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here