Home LOCAL WILAYA YA KAKONKO  YAKUSANYA ZAIDI YA MIL.900 KUPITIA SEKTA YA MADINI

WILAYA YA KAKONKO  YAKUSANYA ZAIDI YA MIL.900 KUPITIA SEKTA YA MADINI

Dodoma

Imeelezwa kuwa , katika kipindi cha kuanzia Mwaka 2019 hadi 2023 jumla ya shilingi 924,685,884 zilikusanywa kutokana na madini yaliyozalishwa katika Wilaya ya Kakonko, mkoani Kigoma.

Hayo yamesemwa leo Agosti 30, 2024 na Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na Mhe. Aloyce John Mbunge wa Buyungu aliyetaka kujua kiasi cha fedha zilipopatikana kutokana na madini katika Wilaya ya Kakonko kuanzia Mwaka 2019 hadi 2023.

Akijibu swali , Dkt. Kiruswa amesema kuwa , Wilaya ya Kakonko ni miongoni mwa Wilaya zilizojaliwa kuwa na madini ya dhahabu nchini.

Kutokana na madini yanayozalishwa Kakonko Shilingi 725,171,133.52 zilitokana na mrabaha na Shilingi 199,514,750.46 zilitokana na ada ya ukaguzi wa madini yaliyozalishwa kwa kipindi kinachorejewa” amesema Dkt. Kiruswa.

Aidha, Dkt. Kiruswa ameongeza kuwa, Madini mengine yanayopatikana katika Wilaya hiyo ni madini ujenzi aina ya mchanga , chuma, Shaba, makaa ya mawe na chokaa ambayo kwa sehemu yamechangia katika ujenzi wa barabara zinazounganisha Wilaya hiyo na maeneo mengine nchini. 

Mkoa wa Kigoma umeunganishwa na wilaya nane , kakonko, kasulu, kibondo , uvinza, Buhigwe, Kusulu vijijini , Kigoma mjini na kigoma vijijini.

#InvestInTanzaniaMiningSector
#Vision2030: MadininiMaisha&Utajiri

Previous articleKATIBU MKUU GERSON MSIGWA AIPONGEZA BENKI YA BIASHARA TANZANIA (TCB) KUUNGA MKONO WADAU WA SANAA
Next articleTTCL KUSAMBAZA INTANETI KATIKA MAENEO YA UMMA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here