NA: JEREMIA ERNEST
WABUNIFU wa mavazi 30 wanatarajiwa kuchuana vikali katika jukwaa moja la Stara Fashion Week, kwa kuonyesha kazi zao kuanzia June 1 hadi 2 katika ukumbi Le Maraheb Masaki Chole jijin Dae Es Salaam.
Huu ni msimu wa nne wa tamasha hili ambao utakutanisha wabunifu kutoka sehemu mbalimbli ndani ya nchi na nje ya Tanzania kuonyeshaa umahiri wao katika mavazi yenye stara.
Akizungumza na ukurasa huu moja ya wasisi wa tamasha hilo Asma Makau, amesema jukwaa hilo ni mahususi kwa kuonyesha nguo zenye kujistri na kutoa frusa kwa wabunifu kujitangaza.
“Hii ni frusa kwa wabunifu wetu wa Afrika kuonyesha kazi zao ambazo zimekuwa na wadau wengi kutokana na tamasha hili pia imekuwa ni sehemu ya kuwakutanisha wabunifu na wateja pamoja na kutanua wigo kwa kukutana na wabunifu wakubwa kutoka nje ya Tanzania,” anasema Asma Makau.
Aliongeza kuwa mwaka huu kuna wabunifu 30 ambao 15 wataonyesha siku ya kwanza na 15 watafunga siku ya pili ambayo ita ambatana na utoaji tuzo kwa wadau, wabunifu na wanamitindo katika vipengele tofauti.