Na:Saimon Mghendi ,KAHAMA.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati, amewataka wananchi wilayani Kahama mkoani Shinyanga kwa Ujumla Kusherekea sikukuu ya Eid al-Adha kwa amani na utulivu sambamba na kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa Corona ikiwa ni Pamoja na kufuata maelekezo yote yanayotolewa na wizara ya afya.
Dkt. Sengati Ameyasema hayo wakati akishiriki ibada ya Eid al-Adha, Iliyofanyika katika Msikiti wa Jumuiya ya kiislamu ya Ahmadiya katika kata ya Zongomela Manispaa ya Kahama, ibada ambayo iliambatana na sadaka ya kitoweo kwa makundi mbali mbali ya watu ikiwa ni muendelezo wa sadaka inayotolewa na Jumuiya hiyo kila mwaka katika sikukuu ya Eid al-Adha.
Aidha Dkt. Sengati Ameishukuru Jumuiya ya Kiislamu ya Ahmadiya kwa Kuwahudumia watu kiroho Pamoja na kimwili na kusema kuwa serekali inathamini mchango wao.
Kwa upande wake Shekh mkuu wa Mkoa Imran Mahmood, Pamoja na Rais wa Mkoa wa Jumuiya hiyo Yousuf Mgeleka, Wamemshukuru Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Pamoja na wanajumuiya wote kwa kuungana Pamoja katika sadaka hiyo.