Home LOCAL MKUU WA MKOA WA SHINYANGA AWATAKA WATU KUSHEREKEA EID KWA AMANI PAMOJA...

MKUU WA MKOA WA SHINYANGA AWATAKA WATU KUSHEREKEA EID KWA AMANI PAMOJA NA KUCHUKUA THADHARI YA CORONA

Na:Saimon Mghendi ,KAHAMA.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati, amewataka wananchi wilayani Kahama mkoani Shinyanga kwa Ujumla Kusherekea sikukuu ya Eid al-Adha kwa amani na utulivu sambamba na kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa Corona ikiwa ni Pamoja na kufuata maelekezo yote yanayotolewa na wizara ya afya.

Dkt. Sengati Ameyasema hayo wakati akishiriki ibada ya Eid al-Adha, Iliyofanyika katika Msikiti wa Jumuiya ya kiislamu ya Ahmadiya katika kata ya Zongomela Manispaa ya Kahama, ibada ambayo iliambatana na sadaka ya kitoweo kwa makundi mbali mbali ya watu ikiwa ni muendelezo wa sadaka inayotolewa na Jumuiya hiyo kila mwaka katika sikukuu ya Eid al-Adha.

Aidha Dkt. Sengati Ameishukuru Jumuiya ya Kiislamu ya Ahmadiya kwa Kuwahudumia watu kiroho Pamoja na kimwili na kusema kuwa serekali inathamini mchango wao.

Kwa upande wake Shekh  mkuu wa Mkoa Imran Mahmood, Pamoja na Rais wa Mkoa wa Jumuiya hiyo Yousuf Mgeleka, Wamemshukuru Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Pamoja na wanajumuiya wote kwa kuungana Pamoja katika sadaka hiyo. 

Previous articleRAIS SAMIA ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA MAMA MGHWIRA
Next articleHABARI KUU ZILIZOPO MAGAZETINI IJUMAA YA LEO JULAI 23-2021

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here