Home LOCAL WAZIRI MKUU APOKEA TAARIFA YA KAMATI KUCHUNGUZA MOTO SOKO LA KARIAKOO

WAZIRI MKUU APOKEA TAARIFA YA KAMATI KUCHUNGUZA MOTO SOKO LA KARIAKOO

DAR ES SALAAM.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo, Julai 27, 2021 amepokea taarifa ya Kamati ya   Uchunguzi wa tukio la moto uliotokea katika soko la kimataifa la Kariakoo tarehe 10 Julai, 2021 jijini Dar es salaam.

Mheshimiwa Majaliwa amepokea taarifa hiyo kutoka kwa mwenyekiti wa Kamati  hayo, CP Liberati Sabas na kuahihidi kuwa serikali itayafanyia kazi mapendekezo yote yaliyotolkewa na Kamati hiyo.
 
Akizungumza baada ya kuipokea taarifa hiyo kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam, Mheshimiwa Majaliwa    amewashukuru na amewapongeza wajumbe wa Tume hiyo kwa kazi nzuri iliyofanyika kwa weledi mkubwa.
 
Mheshimiwa Majaliwa amesema ataifikisha  taarifa hiyo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwani tukio hilo limewagusa watu ndani na nje ya nchi.
 
“Naahidi mbele yako Mwenyekiti kuwa Serikali imeridhishwa na taarifa mlioyo nikabidhi leo na mapendekeso yote mliyoyatoa yatazingatiwa.

Jumapili Julai 11, 2021 Mheshimiwa Majaliwa alipotembelea na kukagua hatua zinazoendela kuchukuliwa kudhibiti moto katika soko la kimataifa la Kariakoo alitangaza kamati ambayo ilipewa kazi ya kuchunguza tukio hilo ili kubaini chanzo cha moto huo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo CP Liberati Sabas amezishukuru Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na wajumbe wengine katika timu hiyo kwa ushirikiano walioutoa katika kufanikisha kazi hiyo “Mheshimiwa Waziri Mkuu kama haya tuliyoyabaini yakifanyiwa kazi matukio kama hayo hayatajirudia”

kamati hiyo aliyoundwa ambayo ilifanya kazi na kamati ya ulinzi na usalama iliyoanza kufanya kazi chini ya Mkuu wa Mkoa huo ilijumuisha  Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Ofisi ya Waziri Mkuu (Idara ya Maafa).

Wengine ni Vyombo vya Ulinzi na Usalama ikujumuisha Jeshi la Wananchi, Jeshi la Polisi, Zimamoto, Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU). Pia Waziri Mkuu alizitaja Wakala wa Majengo, Shirika la Umeme (TANESCO), Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na Ofisi ya Taifa ya mashtaka, Wakala wa Umeme na Ufundi Tanzania (TEMESA)

Previous articleMBUNGE WA SEGEREA BONAH AIPONGEZA SERIKALI KUMPATIA FEDHA ZA KUJENGA SHULE LIWITI
Next articleOFISI YA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS ZANZIBAR, MEYA JIJI LA ZANZIBAR KUSHIRIKIANA KUIRUDISHA ZANZIBAR KWENYE HADHI YAKE.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here