Home LOCAL MBUNGE WA SEGEREA BONAH AIPONGEZA SERIKALI KUMPATIA FEDHA ZA KUJENGA SHULE...

MBUNGE WA SEGEREA BONAH AIPONGEZA SERIKALI KUMPATIA FEDHA ZA KUJENGA SHULE LIWITI

Meya wa Halmashauri ya Jiji La Dar es Salaam Omary Kumbilamoto(kushoto) akizungumza na Mbunge wa Segerea Bonah Ladslaus Kamoli katika ziara ya jimbo iliyoandaliwa na mbunge Leo Julai 26/2021 Kata ya Liwiti kukagua Miradi ya maendeleo(Katikati)Mtendaji wa Kata ya Liwiti Iginas Maembe Diwani wa Liwiti Alice Mwangomo na Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa Liwiti Arafa Mshana(PICHA NA HERI SHAABAN).


Mbunge wa Jimbo LA Segerea Bonah Ladslaus Kamoli (Kulia wa pili)akipata maelezo kutoka kwa Afisa Tarura Wilaya ya Ilala Sililo Joseph leo Julai 26/2021 kusiana na maendeleo ya Daraja la Kipunguni Banana ambalo limegharimu Shilingi milioni 250 (Kushoto kwa Mbunge)Diwani wa Kipawa Aidan Kwezi na Diwani wa Viti Maalum Wilaya ya Ilala MH,Cheka .katika ziara ambayo imeandaliwa na Mbunge kukagua miradi ya Jimbo la Segerea(PICHA NA HERI SHAABAN)


Mbunge wa Jimbo la Segerea Bonah Ladslaus Kamoli (Kulia wa pili) akiwa katika ziara ya Jimbo Kata ya Segerea kukagua miradi wa kituo cha Daladala Segerea ambao umefungwa Taa kwa fedha za Jimbo (kushoto )kwa Mbunge Diwani wa Segerea Robart Manangwa (PICHA NA HERI SHAABAN).
Kheri Shaaban: Afisa TARURA Wilaya ya Ilala Sililo Joseph (kulia)akiwa katika msafara wa Mbunge wa Segerea (katikati)Bonah Ladslaus Kamoli kukagua Barabara ya Vingunguti Barakuda leo Julai ,26/2021 (Kushoto)Meya wa Dar es Salaam Omary Kumbilamoto(PICHA NA HERI SHAABAN
 
Na: HERI SHAABAN (ILALA).

MBUNGE wa Jimbo la Segerea Bonah Ladslaus Kamoli ameipongeza Serikali kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Sekondari ya Serikali ambayo itajengwa Liwiti .

Mbunge Bonah aliyasema hayo Dar es Salaam Jana katika mwendelezo wa ziara zake za kutembelea miradi ya serikali na kutatua kero za Wananchi.

“Kata ya Liwiti miongoni mwa kata iliyokosa shule ya sekondari miaka yote  naipongeza Serikali yangu kunipatia fedha sekta ya Elimu iweze kukua tunatarajia kuanza ujenzi wa Shule  mpya ili watoto wasiende mbali “ alisema Bonah

Mbunge Bonah alisema ziara hiyo ni mwendelezo wa  ziara zake  amekua akiifanya katika Jimbo hilo, ambapo leo ametembelea Kata ya Segerea, Liwiti, Vingunguti pamoja na Kipawa na kukagua miradi mbalimbali ikiwemo Ujenzi wa daraja barabara ya Banana kitunda, barabara ya Vingunguti Barakuda pamoja na taa za stendi ya Segerea.

Aidha, amesema kuwa, ameridhishwa na Ujenzi wa miradi ya Maendeleo katika Jimbo hilo ambapo amesema miradi hiyo inatekelezwa kwa pesa za Serikali kuu pamoja mfuko wa Jimbo.

Kwa upande wake,Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Liwiti  Arafa Shamna amesema kuwa, kuwepo kwa shule ya Sekondari katika kata hiyo itakua msaada mkubwa na kupunguza adha ya usafiri wanayoipata wanafunzi kwenda umbali mrefu ikiwemo Kata ya Chanika, Zingiziwa, Minazi Mirefu pamoja na Segerea.

Naye, Diwani wa kata ya Liwiti Alice Mwangomo amesema anaishukuru Serikali kwa kuingalia barabara ya Vingunguti barakuda kwani barabara hiyo inaunganisha wakazi wa Segerea na Vingunguti na Maeneo ya jirani.

Katika hatua nyengine, Diwani wa Kata ya Kipawa Aidan Kwezi amesema kuwa kata hiyo inatarajiwa kuwa na miradi mingi ya Maendeleo ikiwemo ujenzi wa daraja katika barabara ya Banana kitunda ambao  umekamilika kwa asilimia kubwa.

“Barabara ya Uwanja Ndege , Karakata nayo pia inatarajiwa kujengwa kwa kiwango cha lami ambapo ujenzi utaanza muda si mrefu kwani wananchi wamekua wakipata shida kubwa kutokana na barabara hiyo sio rafiki kwao”alisema Aidan.

Aidha, Mtendaji wa Kata ya Segerea Eligius Mulokozi alisema mpaka sasa kata hiyo imeshapokea zaidi ya sh, mill 60 kwa ajili ya miradi ya Maendeleo ikiwemo taa za stendi ya Segerea,ukarabati wa barabara pamoja na ukarabati wa vyumba vya madarasa upande wa sekta ya elimu.

Mwisho

Previous articleMAONESHO YA 16 YA TCU YAZINDULIWA RASMI LEO, VYUO VYAFANYA UDAHILI WA MOJA KWA MOJA KWENYE MABANDA YAO DAR.
Next articleWAZIRI MKUU APOKEA TAARIFA YA KAMATI KUCHUNGUZA MOTO SOKO LA KARIAKOO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here