Home LOCAL RAIS SAMIA AZINDUA SHULE YA MAANDALIZI TASANI

RAIS SAMIA AZINDUA SHULE YA MAANDALIZI TASANI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Tamasha la Kizimkazi limeendelea kujipambanua kuwa laki maendeleo kwa kuchochea utekelezaji wa miradi ya maendeleo yenye manufaa makubwa kwa wananchi.

Rais Dkt. Samia amesema hayo wakati akifungua Skuli ya Maandalizi Tasani iliyoko Makunduchi na kusisitiza kuwa njia nzuri ya kuwalinda watoto ni kuuhakikisha kuwa wanapata fursa ya kusoma.

 

Aidha, Rais Dkt. Samia amewataka walezi wa kituo hicho kuwalea watoto kimaadili na kiakili kwa kuzingatia misingi ya Malezi ya Awali ya Mtoto (ECD).

Rais Dkt. Samia amesema Serikali ina dhamira ya kuhakikisha kwamba watoto wote nchini wanapata malezi bora ikiwemo maandalizi mazuri yatakayowapa msingi mzuri wa mafanikio shuleni na maishani.

Katika hafla ya kuhitimisha mafunzo na kugawa vyeti kwa washiriki wa mafunzo ya ujasiriamali, Rais Dkt. Samia amewataka vijana kuchangamkia fursa za kupata mafunzo na ujuzi mbalimbali ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Rais Dkt. Samia pia amewataka wahitimu waliopata mafunzo kufanya shughuli za kiuchumi za kilimo, utalii na uvuvi huku wakitunza mazingira, mila na desturi ambazo ndizo zinawavutia watalii kuja Zanzibar.

Kupitia Tamasha la Kizimkazi jumla ya vijana 607 wamepati wamafunzo ya ujasiriamali pamoja na kilimo, uvuvi mifugo, utalii na sanaa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Tamasha la Kizimkazi la mwaka 2024.

Previous articleBARRICK YAKABIDHI GAWIO LA MRAHABA VIJIJI 5 WILAYANI TARIME
Next articleWAPENI MADEREVA STAHIKI ZAO – MAJALIWA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here