Postamasta Mkuu Mstaafu wa Shirika la Posta Tanzania Ndugu Deus Mmdeme akizungumza jambo wakati wa kufunga kikao hicho |
Na:Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM
Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Kundo Andrea Mathew (Mb) amewataka Mameneja wa Mikoa na wale wa Makao Makuu ya Shirika la Posta Tanzania kutekeleza yale waliyoazimia kwenye kikao cha kutathmini utendaji kazi wa Viongozi wa Shirika la Posta Tanzania kwa mwaka uliopita 2020/2021 na kukubalina malengo kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
Mhandisi Kundo ameyasema hayo tarehe 6 Agost 2021, Jijini Dar e’s Salaam, alipokuwa akifunga rasmi kikao kazi hicho cha siku tano ambacho pamoja na mambo mengine kilijadili Mpango Mkakati wa Shirika kwa mwaka 2021/2022.
“Mliyokubaliana hapa mkayatekeleze kwa pamoja kwa kuzingatia weledi na nidhamu ndani ya Shirika” alizungumza Mhandisi Kundo.
Aidha Naibu Waziri Kundo aliwataka viongozi Wakuu wa Shirika kuwawezesha vifaa vya kisasa Mameneja wa Mikoa na Kuwapa wigo mpana na uhuru wa kutekeleza majukumu yao ya kazi badala ya Makao Makuu kuwa msemaji wa mwisho utekelezaji wa majukumu ya Shirika katika Mikoa yao.
Nae Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Ndugu Macrice Daniel Mbodo alielezea namna Viongozi hao wa Shirika walivyopata semina mbalimbali za Itifaki “Protocol”, Matumizi ya mifumo ya Shirika ya Teknolojia, pamoja na uwajibikaji pamoja na utendaji ndani ya Shirika.
Ndugu Mbodo amemshuru Naibu Waziri Kundo kwa kuweza kufika na kufunga kikao hicho na kuahidi kutafanyia kazi ile mikakati waliyojiwekea pamoja na yale yaliyoagizwa na Wizara kwa maendeleo ya Shirika.
Aidha kikao hicho kilichohudhuriwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu Mstaafu wa Hesabu za Serikali, Ndugu Ludovick Utouh na Postamasta Mkuu Mstaafu wa Shirika la Posta Tanzania Ndugu Deus Mmdeme.
Imetolewa na;
OFISI YA MAWASILIANO
SHIRIKA LA POSTA TANZANIA.