Home LOCAL NENDENI MKAYATEKELEZE MLIYOYAAZIMIA KWENYE KIKAO KAZI- MHANDISI KUNDO.

NENDENI MKAYATEKELEZE MLIYOYAAZIMIA KWENYE KIKAO KAZI- MHANDISI KUNDO.

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Habari, Mhe. Mhandisi Kundo Andrea Mathew akizungumza wakati wa kufunga kikao kazi cha kutathmini utendaji kazi wa Viongozi wa Shirika la Posta Tanzania kwa mwaka uliopita 2020/2021 na kukubalina malengo kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Kundo A. Mathew akiteta jambo na Kaimu Postamasta Mkuu Macrice Daniel Mbodo wakati wa kufunga kikao kazi cha Viongozi wa Shirika la Posta Tanzania, leo jijini Dar es Salaam.

Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta, Bwana Macrice Mbodo, akizungumza wakati wa kufunga kikao kikao kazi cha kutathmini utendaji kazi wa Viongozi wa Shirika la Posta Tanzania kwa mwaka uliopita 2020/2021 na kukubalina malengo kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu Mstaafu Hesabu za Serikali, Ndugu Ludovick Utouh akizungumza wakati wa kufunga kikao kazi hicho.

Postamasta Mkuu Mstaafu wa Shirika la Posta Tanzania Ndugu Deus Mmdeme akizungumza jambo wakati wa kufunga kikao hicho

Viongozi mbalimbali wa Shirika la Posta pichani wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Andrea Mathew (Mb).

Kaimu Postamasta Mkuu, Ndugu Macrice Mbodo akisisitiza Jambo.

Na:Mwandishi  wetu, DAR ES SALAAM 

Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Kundo Andrea Mathew (Mb) amewataka Mameneja wa Mikoa na wale wa Makao Makuu ya Shirika la Posta Tanzania kutekeleza yale waliyoazimia kwenye kikao cha kutathmini utendaji kazi wa Viongozi wa Shirika la Posta Tanzania kwa mwaka uliopita 2020/2021 na kukubalina malengo kwa mwaka wa fedha 2021/2022. 

Mhandisi Kundo ameyasema hayo tarehe 6 Agost 2021, Jijini Dar e’s Salaam,  alipokuwa akifunga rasmi kikao kazi hicho cha siku tano ambacho pamoja na mambo mengine kilijadili Mpango Mkakati wa Shirika kwa mwaka 2021/2022. 

“Mliyokubaliana hapa mkayatekeleze kwa pamoja kwa kuzingatia weledi na nidhamu ndani ya Shirika” alizungumza Mhandisi Kundo. 

Aidha Naibu Waziri Kundo aliwataka viongozi Wakuu wa Shirika kuwawezesha vifaa vya kisasa Mameneja wa Mikoa na Kuwapa wigo mpana na uhuru wa kutekeleza majukumu yao ya kazi badala ya Makao Makuu kuwa msemaji wa mwisho utekelezaji wa majukumu ya Shirika katika  Mikoa yao. 

Nae Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Ndugu Macrice Daniel Mbodo alielezea namna Viongozi hao wa Shirika walivyopata semina mbalimbali za Itifaki “Protocol”, Matumizi ya mifumo ya Shirika ya Teknolojia, pamoja na uwajibikaji pamoja na utendaji ndani ya Shirika.

Ndugu Mbodo amemshuru Naibu Waziri Kundo kwa kuweza kufika na kufunga kikao hicho na kuahidi kutafanyia kazi ile mikakati waliyojiwekea pamoja na yale yaliyoagizwa na Wizara kwa maendeleo ya Shirika.

Aidha kikao hicho kilichohudhuriwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu Mstaafu wa Hesabu za Serikali, Ndugu Ludovick Utouh na Postamasta Mkuu Mstaafu wa Shirika la Posta Tanzania Ndugu Deus Mmdeme. 

Imetolewa na;

OFISI YA MAWASILIANO 

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA.

Previous articleWAZIRI AWATAKA WALIMU WAKUU NA WALIMU WA TEHAMA KUTOZIFUNGIA KOMPYUTA KWENYE MAKABATI.
Next articleRC MAKALLA AHIMIZA WANANCHI KUFANYA MAZOEZI.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here