Home BUSINESS EPZA YAHAMASISHA WAWEKEZAJI WANDANI KUTUMIA FURSA WALIZONAZO

EPZA YAHAMASISHA WAWEKEZAJI WANDANI KUTUMIA FURSA WALIZONAZO

Na; HUGHES DUGILO, DODOMA

Serikali kupitia Mamlaka ya Uwekezaji EPZA imeendeleza jitihada zake za kuhakikisha wawekezaji wazawa wanapata fursa ya kuzalisha bidhaa zinazokidhi soko la nje ili kuiongezea nchi pesa za kigeni.

Hayo yameelezwa na Kaimu Meneja wa uhamasishaji wa EPZA BI. Nakadongo Phares, alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane-nane yanayoendelea kwenye viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.

‘Tuko hapa Nane-nane kutoa elimu kwa wananchi, lakini pia kuelezea fursa zilizopo za kupata maeneo maalum katika fursa za uwekezaji wa viwanda vinavyozalisha kupeleka nje ya nchi’ amesema Bi. Nakadongo.

Amesema kuwa EPZA ina programu ya kumuwezesha mwekezaji kupata leseni itakayopelekea kupata eneo maalum nakuanza ujenzi wa kiwanda lengo likiwa ni kuuza nje kwa asilimia 80 na ndani asilimia 20.

Aidha Mwekezaji hajazuiliwa kufanya mauzo nje kwa asilimia 100

Pia, amefafanua kuwa Leseni anayoipata mwekezaji inamuwezesha kupatiwa eeneo maalum lililoboreshwa tayari kwa uwekezaji.

Maeneo hayo yapo Bagamoyo Pwani, Manyara, Mtwara na Tanga, pamoja na sehemu nyinge nchini, atapatiwa ili kuanza ujenzi wa kiwanda chake.

‘Kwahiyo ninawahamasisha wawekezaji wetu wa ndani kuweza kutumia fursa hizi kwenye maeneo yetu maalum ya uwekezaji wa viwanda. Tusiache hii fursa ikatumiwa na watu wa nje’ amesema Bi. Nakadongo.

Malengo ya kisera ya uanzishwaji wa programu ya EPZ na SEZ yaliyoanishwa kwenye kifungu cha 4 cha Sheria ya EPZ, Sura 373 na kifungu cha 5 cha Sheria ya SEZ, Sura 420 ni pamoja na Kujenga uwezo wa sekta ya viwanda kuzalisha ushindani wa masoko kibiashara ndani na nje ya Tanzania;

Previous articleBoT KUSAIDIA WAJASIRIAMALI KUPITIA MFUKO WA UDHAMINI WA MIKOPO – (ECGS)
Next articleBoT: TAASISI ZA FEDHA ZINAPASWA KUWAKOPESHA WAKULIMA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here