Home BUSINESS BoT KUSAIDIA WAJASIRIAMALI KUPITIA MFUKO WA UDHAMINI WA MIKOPO – (ECGS)

BoT KUSAIDIA WAJASIRIAMALI KUPITIA MFUKO WA UDHAMINI WA MIKOPO – (ECGS)

Mchambuzi Mwandamizi wa Masuala ya Fedha Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Gloria  Samwel Chellunga, akizungumza na waandishi wa Habari kwenye Maonesho ya Nnane-nane yanayofanyia kwenye viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.

DODOMA

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imejipanga kuwasaidia Wajasiriamali nchini kupitia Mfuko wa Udhamini wa Mikopo kwa ajili ya Mauzo Nje ya Nchi (ECGS) pamoja Mfuko wa Udhamini wa Mikopo kwa Wajasiriamali Wadogo na wa Kati (SME-CGS) ikiwa na lengo la kuwezesha wakopaji wenye miradi mizuri kwa ajili ya kuweza kupata mitaji kutoka kwenye mabenki na taasisi za fedha, pale wanapokuwa na upungufu wa dhamana ambayo inatoa fursa ya udhamini.

Akizungumza leo Agusti 5, 2024 katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayofanyika Nzuguni jijini Dodoma, Mchambuzi Mwandamizi wa Masuala ya Fedha Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Gloria  Samwel Chellunga, amesema kuwa BoT wanasimamia mfuko wa udhamini wa mkopo kwa niaba ya serikali ili kuwasaidia watanzania.

Chellunga amesema kuwa mfuko wa udhamini wa mikopo kwa wajasiriamali wadogo na wa kati kwa ajili ya kuwawezesha wajasiriamali wenye miradi mizuri lakini wana upungufu wa dhamana, kuweza kupata mitaji kutoka kwenye mabenki na taasisi za fedha.

“mfuko huu unatoa udhamini usiozidi asilimia 50 kwa mikopo kati ya shilingi milioni 50 hadi shilingi bilioni moja itakayotolewa kwa kipindi kati ya mwaka 1 hadi 5..

“Mikopo kwa ajili ya Mauzo Nje ya Nchi umelenga kuwezesha wakopaji wenye miradi mizuri kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa na mauzo nje ya nchi, kuweza kupata mitaji kutoka kwenye mabenki na taasisi za fedha, pale wanapokuwa na upungufu wa dhamana“ amesema Chellunga

Aidha ameongeza kuwa udhamini wa mikopo katika mfuko huu hauzidi asilimia 75 kwa mkopo unaolipika ndani ya mwaka mmoja; na asimilia 50 ya mkopo kwa mkopo unaolipika zaidi ya mwaka mmoja.

“Kwa mkopo wa mazao ambayo mzunguko wa uzalishaji na uuzaji wake unazidi miezi kumi na mbili (12) lakini si zaidi ya miezi kumi na tano (15), udhamini wa mkopo hautazidi asilimia 75” ameongeza.

Amesema kuwa lengo ni kusaidia sekta binafsi pamoja na wajasilimali wadogo wenye miradi mzuri na kupata mikopo kutoka benki au taasisi za fedha zinazosimamiwa na benki kuu ambao wamepungukiwa na dhamana.

Amefafanua kuwa ili uweza kupata dhamana katika mifuko huo, mwombaji ambaye ni mjasiliamali mdogo akiwemo mvuvi au mkulima anatakiwa kutuma maombi katika benki yake akiwa na andiko linaloelezea mradi wake.

Amefafanua kuwa benki itafanya tathmini ya mkopo huo kwa kuzingatia sera, huku benki husika itatuma maombi BoT kwa ajili ya kupata dhamana kwa ajili ya kumkopesha mteja wake.

  

Previous articleTMDA YATOA ELIMU KWA WANANCHI UTUMIAJI NA UTUNZAJI SAHIHI WA DAWA
Next articleEPZA YAHAMASISHA WAWEKEZAJI WANDANI KUTUMIA FURSA WALIZONAZO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here