Home BUSINESS NAIBU WAZIRI NDERIANANGA AMPONGEZA STAMICO KUWEZESHA MAKUNDI MAALUM

NAIBU WAZIRI NDERIANANGA AMPONGEZA STAMICO KUWEZESHA MAKUNDI MAALUM

 

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Uratibu na Bunge) Mhe. Ummy Nderiananga amelipongeza Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwa kuwezesha makundi maalumu kushiriki katika uvunaji wa rasilimali madini.

Pongezi hizo amezitoa Agosti 4, 2024 kwenye banda la STAMICO alipokutana na makundi hayo wakishiriki Maonesho ya Nane Nane kupitia Shirika yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.

Mhe. Ummy amesema amevutiwa na namna STAMICO inavyobuni miradi na kushirikisha makundi haya katika sekta ya madini jambo linalowawezesha kujipatia kipato.

“Nawashukuru na kuwapongeza STAMICO kwa kuwaibua na kuwasaidia watu wa makundi maalumu na kuwashirikisha katika miradi ya kimaendeleo, endeleeni kuwashirikisha pia katika shughuli zingine kama vile uzalishaji wa vifungashio
Ili kuwaletea mwamko wa kiuchumi” Aliongeza Mhe. Ummy

Amewataka wanufaika wa miradi hiyo kuhakikisha wanatumia fursa vizuri ili iweze kuwanufaisha watu wengi wenye mahitaji maalum kwa kuwa STAMICO wamefanya jambo nzuri kuhakikisha watu wenye makundi maalumu wanashiriki kwenye uchumi jumuishi.

Akizungumza kwa upande wake, Afisa Uhusiano wa STAMICO Bi. Bibiana Ndumbaro amesema Shirika litaendelea kuhakisha kila mtanzania ananufaika na rasilimali madini kwa kushiriki kwa namna moja au nyingine kwenye shughuli zote zinazofanyika katika mnyororo wa thamani wa madini zikiwemo za Utafiti, uchimbaji, uchenjuaji, uongezaji thamani na biashara ya madini.

Amesema Shirika limewezesha makundi mbalimbali yakiwemo Taasisi ya Maendeleo ya Viziwi Tanzania (TAMAVITA) kwenye kuchimba madini, kuwapa uwakala wa kuuza nishati mbadala ya kupikia ya Rafiki Briquettes Taasisi ya kusaidia Watu wenye Ulemavu (FDH) pamoja na Wanawake na Samia Dodoma, Sambamba na kuwajengea ofisi na kuwapatia mtaji wa kuanza biashara ya kuuza nishati hiyo.

Akiongea kwa niaba ya watu wenye ualbino mwakilishi kutoka FDH, Bw. Miraji Msingwa ameelezea manufaa ya ufadhili wanaoupata kutoka STAMICO kuwa unawawezesha kujipatia kipato pamoja na kuwasaidia wenzao wasiojiweza wenye uhitaji wa vifaa tiba kwa ajili ya ngozi.

Amesema ni fursa kwao kushiriki kuhamasisha utunzaji wa mazingira kupitia Rafiki Briquettes jambo litakaloepusha ukataji wa miti ovyo hivyo kupunguza ongezeko bla hewa ukaa.

“Tunaishukuru STAMICO kushirikisha watu wenye ulemavu hasa watu wenye ualbino kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala ya kupikia kwa sababu sisi ndio wahanga wakubwa wa jua hivyo uwepo wa mkaa huu utasaidia upatikanaji wa vivuli kwa wingi na kuokoa watu wenye ualbino kutoathirika na kansa ya ngozi kwa kuepuka mionzi ya jua.” Alisema Miraji.

Aidha, Mwenyekiti wa Kikundi cha Wanawake na Samia Bi. Fatuma Madidi wameishukuru STAMICO kuendelea kuwashika mkono katika kufanya biashara ya nishati mbadala.

“Tunawashukuru sana STAMICO kwa kujali makundi mbalimbali katika jamii na kuwainua kiuchumi, sisi ni wanufaika wa mradi huu wa nishati mbadala ya kupikia na tunahamasisha utunzaji wa mazingira” Alisitiza Madidi.

STAMICO imeendelea kutoa hamasa ya matumizi ya nishati mbadala ya kupikia ili kutunza misitu na kuhifadhi vyanzo vya maji.

Previous articleKATIBU MKUU WA CCM Dkt. NCHIMBI ATOA MAELEKEZO KWA MAWAZIRI
Next articleNMB FOUNDATION, ZASCO WAZINDUA MAFUNZO YA WAKULIMA WA MWANI ZANZIBAR
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here